Waziri wa ulinzi wa Uturuki azungumza na  makamu  mwenyekiti wa baraza la maridhiano Libya

Waziri wa ulinzi wa Uturuki azungumza na  makamu  mwenyekiti wa baraza la maridhiano Libya

1491775
Waziri wa ulinzi wa Uturuki azungumza na  makamu  mwenyekiti wa baraza la maridhiano Libya


Waziri wa ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar amezungumza na makamu mwenye kiti wa baraza  la maridhiano wa serikali ya Libya kuhusu   hali inayoendelea nchini Libya.

Makumu huyo  wa baraza la  maridhiano  nchini Libya amesema kuwa matumaini  ya taifa lake ni kuwa kama ilivyokuwa hapo awali.

Ahmet Maiteek amezungumzo na waziri wa ulinzi wa Uturuki  kuhusu pia masuala ya kikanda na hali inayoendelea nchini Libya licha ya kudhoofishwa vikosi vya wanamgambo waliokuwa wakiendesha mashambulizi nchini humo.

Katika mazungumzo yao, wairi wa ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar amekumbusha mwamba Uturuki na Libya ni mataifa rafiki kwa kipindi cha miaka zaidi ya  500.

Akar ameendelea akifahamisha kuwa Uturuki itaendelea kuwa bega kwa bega na Libya na kuendelea na msimamo wake   wa kuunga mkono harakati za serikali halali ya Libya inayotambuliwa na Jumuiya ya kimataifa katika  elimu na usalama.

Kwa kumalizia , waziri wa ulinzi wa Uturuki  amefahamisha kuwa Uturuki ipo tayari kuendelea kushirikiana na Libya kwa hali na mali hadi pale ambapo Libya itakapofikia  malengo yake.

 Habari Zinazohusiana