Mradi wa treni ya umeme nchini Uturuki

Waziri wa Uchukuzi na Miundombinu wa Uturuki Adil Karaismailoğlu amesema kwamba treni ya kwanza ya umeme kutengenezwa Uturuki inatarajia kuingia relini mwishoni mwa mwaka huu

1445522
Mradi wa treni ya umeme nchini Uturuki
milli tren 2.jpg
milli tren 1.jpg

Waziri wa Uchukuzi na Miundombinu wa Uturuki Adil Karaismailoğlu amesema kwamba treni ya kwanza ya umeme kutengenezwa Uturuki inatarajia kuingia relini mwishoni mwa mwaka huu.

Karaismailoğlu, katika hotuba yake katika hafla hiyo ambapo majaribio ya kiwanda cha treni ya umeme yatazinduliwa huko Sakarya, amesema kwamba wameazimia kuendelea na utaalam katika teknolojia ya reli na utengenezaji wa magari ya ndani na ya kitaifa,

"Lengo letu ni kuwa reli ya Uturuki ni chombo muhimu katika vituo vya uzalishaji." aliongeza kiongozi huyo.

Akielezea kuwa za treni za ndani na za kitaifa zinatengenezwa kwa kasi ya kufanya kazi ya kilomita 160 kwa saa na kasi ya muundo wa kilomita 176, Karaismailoğlu amesema kuwa ana sifa za kukidhi matakwa na matarajio yake katika kiwango cha usalama wa abiria.

Karaismailoğlu amesema kuwa treni itakuwa ina viti 324 ambapo baadhi ya siti zimehifadhiwa kwa ajili ya walemvu.

Waziri wa Uchukuzi na Miundombinu amesema kuwa mfano huo uliowekwa, ambao uzalishaji wake umekamilika, umetengenezwa kwa kiwango cha asilimia 60 kwa rasiliamali za ndani na asilimia 80 ya kiwango cha uzalishaji mkubwa.

Waziri huyo amemalizia kwa kusema kuwa kwa sasa Uturuki ina uwezo wa kutengeneza treni zake za umeme ndani ya nchi na haina haja tena ya kuwa inanunua kutoka nchi nyingine.

 Habari Zinazohusiana