Uturuki na maambukizi ya virusi vya corona

Watu  27 wamefariki kutokana na maaambukizi ya virusi vya corona Uturuki

1441810
Uturuki na maambukizi ya virusi vya corona


Watu  27 wamefariki kutokana na maaambukizi ya virusi vya corona Uturuki.

Wizara ya afya ya Uturuk imefahamisha kwamba  watu 27 wamefariki ndani ya masaa  24 kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Idadi ya vifo kutokana na  virusi hivyo imeongezeka baada ya watu hao  kuripotiwa kufariki ndani ya masaa  24 na kufikia watu 5001.

Watu 42982 wamepimwa huku ikifahamishwa kwamba watu  1268 wamegunduliwa kuwa na maambukizi ya virusi hivyo.

Watu  315 wameruhusiwa kuondoka hospitali baada ya vipimo kuonesha kuwa hawana maambukizi baada ya kupatiwa  matibabu, idadi ya watu waliopona covid-19 imefikia watu  162848.Habari Zinazohusiana