Uturuki na matumaini  yake katika kukabiliana na virusi vya corona

Uturuki yaendelea   kupambana na maambuizi ya virusi vya corona kwa matumaini

1422205
Uturuki na matumaini  yake katika kukabiliana na virusi vya corona


Uturuki yaendelea   kupambana na maambuizi ya virusi vya corona kwa matumaini.

Idadi ya watu ambao wameathirika na maambukizi ya virusi vya corona nchini Uturuki imeripotiwa kuzidi kupungua kila kukicha.

Ndani ya masaa  24, watu  27 ndio ambao wizara ya afya  ya Uturuki imetangaza kwamba wamefariki kutokana na covid-19.

Idadi hiyo ya vifo kupungua inatoa matumaini kwa wauguzi na madaktari ambao usiku kucha walikuwa wakiteleza majukumu yao.

Madaktari sasa wana matumaini katika jitihada zao za kuzuia maambukizi kuendelea kuwa tishio katika ardhi ya Uturuki.

Baada ya idadi hiyo kutangazwa ndani ya masaa  24, idadi kamili  ya watu ambao wamefariki kote nchini Uturuki tangu kuanza kwa janga hilo imefikia watu  4276.

Watu  37507 wamepimwa huku watu  952 ndio wametangwa kuwa  wamegunduliwa  kuwa na maambukizi.Habari Zinazohusiana