Mauzo ya nyanya yaongezeka nchini Uturuki

Mauzo ya nje ya nyanya nchini Uturuki yameongezeka kwa asilimia 10 katika kipndi cha Januari-Machi mwaka huu ikilinganishwa na kipndi kama hicho mwaka jana.

1395721
Mauzo ya nyanya yaongezeka nchini Uturuki

Mauzo ya nje ya nyanya nchini Uturuki yameongezeka kwa asilimia 10 katika kipndi cha Januari-Machi mwaka huu ikilinganishwa na kipndi kama hicho mwaka jana.

Kulingana na ripoti iliyotolewa,kiwango hicho kimeongezeka na kufikia dola milioni 126,257.

Mauzo ya nje ya Uturuki mwaka jana yalikuwa na thamani ya dola milioni 304,513 baada ya kuuza kwa nchi 56 tofauti.

Kipindi cha kati ya Januari-Machi mwaka jana, mauzo ya nyanya kutoka Uturuki kwenda nchi za nje yalifkia thamani ya dola milioni 114 645 kwa kuuzia nchi 45 tofauti.

Urusi ni kati ya nchi za kwanza zinazonunua nyanya kutoka Uturuki.

Mauzo ya nyanya kati ya Uturuki na Urusi katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu yalifikia thamani ya dola milioni 41,665.

Baada ya Urusi,nchi zinazofuata kwa kununua zaidi nyanya kutoka Uturuki ni Romania ikiwa imenunua kiasi cha nyanya chenye thamani ya dola milioni 18,464ikifuatiwa na UKraine kwa thamani ya dola milioni 13,714.

 Habari Zinazohusiana