Waturuki 124 wamefariki kutokana na Covid-19 wakiwa ugenini

Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki imefahamisha kuwa  idadi ya waturuki waliofariki kwa virusi vya corona wakiwa ugenini imeongezeka

1390230
Waturuki 124 wamefariki kutokana na Covid-19 wakiwa ugenini

Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki imefahamisha kuwa  idadi ya waturuki waliofariki kwa virusi vya corona wakiwa ugenini imeongezeka na kufikia watu 124.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu amefahamisha kuwa amepata taarifa kuhusu idadi ya waturuki ambao wamekwishafariki kutokana na virusi vya corona   wakiwa ugenini.

Çavuşoğlu amesema kuwa waturuki  124 ndio waliofariki .

Hayo ameyazungumza baada ya mkutano wa njia ya video wa mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama wa NATO.

Waturuki  20 000 waliokuwa ugenini wamerejeshwa Uturuki tangu Machi 17  kutokana na kuibuka kwa virusi vya corona.

Raia hao wakituruki walikuwa katika mataifa  50 ulimwenguni.

Taarifa ya waziri wa mambo ya nje wa Uturuki imefahamisha kusikitishwa na vifo vya waturuki   124 ugenini.

Makamu waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Yavuz Selim Kıran amepeperusha ujumbe kuhusu virusi vya corona kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Nchini Ufaransa waturuki 47 ndio waliofariki, Ujerumani 23, Uholanzi 20, Ubelgiji 10, Uingereza  9, Marekani 6,  Uswisi  5, Uswidi 3,  Austria wawili.Habari Zinazohusiana