Uturuki yalaani shambulizi la kigaidi nchini Chad

Uturuki yakemea vikali  shambulizi la kigaidi  lililoendeshwa na wanamgambo wa Boko Haramu nchini Chad

Uturuki yalaani shambulizi la kigaidi nchini Chad


 Uturuki yakemea vikali  shambulizi la kigaidi  lililoendeshwa na wanamgambo wa Boko Haramu nchini Chad.

Wanamgambo wa kundi la Boko Haramu wameendesha  shambulizi la kigaidi na kusababisha vifo vya 92 na kuwajeruhi waengine  47 nchini Chad.

Miongoni watu waliouawa na kujeruhiwa wamo pia wanajeshi.

Uturuki kupitia  wizara yake ya mambo ya nje imelaani vikali shambulizi hilo.

Katika tangazo lake , wizara ya mambo ya nje ya Uturuki imekemea shambulizi hilo la kigaidi liliowalenga wanajeshi  katika kambi yao   karibu na  ziwa Chadi Machi 23 mwaka  2020.

Salamu za rambi rambi  zimetolewa kwa familia za wahanga na taifa zima   huku majeruhi wakitakiwa shifa na kurejea katika  majukumu yao ya kulinda taifa watakapopona.
 


Tagi: Chad , Uturuki

Habari Zinazohusiana