Idadi ya watu ambao wamekwishafariki kutokana na virusi vya corona yaongezeka Uturuki

Idadi ya watu waliofariki kutokana na virusi vya corona nchini Uturuki yarpotiwa kuzidi kuongezeka na kufikia watu  59

1385110
Idadi ya watu ambao wamekwishafariki kutokana na virusi vya corona yaongezeka Uturuki


Idadi ya watu waliofariki kutokana na virusi vya corona nchini Uturuki yarpotiwa kuzidi kuongezeka na kufikia watu  59.

Waziri wa afya wa Uturuki Fahrettin Koca ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na virusi vya corona yazidi kuongezeka na kufikia watu 59.

Katika ujumbe wake huo kupitia ukurasa wake wa Twitter, waziri wa afya wa Uturuki amefahamisha vifo vya watu 15 waliokuwa wamelazwa hospitali kwa virusi vya corona  na kupelekea idadi hiyo kuongezeka na kufikia watu 59.

Katika kipindi cha muda wa masaa 24, watu 5035 wampimwa virusi vua Covşd-19 huku watu 561 matokeo yao yakionesha kwamba wamekwishaathirika na virusi hivyo.

Taarifa nyingine iliotolewa na wizara ya afya  imefahamisha kuwa wagonjwa 26  waliopona baada ya kupatiwa matibabu wameruhusiwa kuondoka hospitali. 

Kwa upande wake waziri wa elimu Ziya Selçlçuk amesema kuwa shule zitandelea kufungwa hadi April 30.
 Habari Zinazohusiana