Kalın  : "Tuwazindue wazee wetu bila kuwabughudhi"

Msemaji wa ikulu ya rais  Ibrahim Kalın  atoa wito wa kuwaheshimu wazee wakati wa kuwzindua kuhusu uhatari wa Covid-19

Kalın  : "Tuwazindue wazee wetu bila kuwabughudhi"


Msemaji wa ikkulu ya rais  Ibrahim Kalın  atoa wito wa kuwaheshimu wazee wakati wa kuwazindua kuhusu uhatari wa Covid-19.

Ibrahim Klaın , msemaji wa   rais mjni Ankara ametolewa wito wa kuwaheshimu wazee wakati wa kuwakumbusha kuwa kubaki kwao nyumbani ni bora kwa afya zao na kuepuka maambukizi ya virusi vya corona.

Kalın katika ujumbe wake  kuhusu wazee kubaki majumbani amesema kuwa ujumbe kwa wazee unatakiwa kutolewa kwa kuheshimu  sheria na  kuheshimu wazee.

Wazee wameomba kubaki majumbani ili   kuwalinda  na kuambukiwa na virusi vya Covid-19.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Ibrahim Kalın  amefahamisha kuwa  watu zaidi ya  13000 wamekwishafariki kutokana na virusi vya corona ulimwenguni, kunatakiwa kuchukuliwa hatua zinazostahili kukabiliana na janga hilo kwa hali na mali.

Ibrahim Kalın ametoa wito pia wa kuheshi  hatua zilizotangazwa na mamlaka husika katika juhudi za kupambana na virusi vya corona katika pembe zote nne za Uturuki.

Nchini Italia watu  zaidi ya  700 wamekwishafariki na kuongoza barani Ulaya kwa kuwa na idadi kubwa ta watu walioathirika na virusi hivyo vya Covid-19 tangu kuanza kwake nchini China mwishoni mwa mwaka  2019.

Kalın amewatahadhari vijana  wanaodhani kuwa si rahisi kuambukiwa virusi hivyo kwa kusema kuwa  wanajiweka hatari  na kuwaweka  watu wengine katika hatari.
 Habari Zinazohusiana