Ushirikiano wa kibiashara biana ya Uturuki na Zambia

Mkutano wa kwanza wa tume ya pamoja ya kiuchumi baina ya Uturuki na Zambia wafanyika mjini Lusaka

Ushirikiano wa kibiashara biana ya Uturuki na Zambia

Mkutano wa kwanza wa tume ya pamoja ya Uchumi baina ya Uturuki na Zambia umefanyika chini ya mwenyekiti mwenza wa waziri wa familia, kazi, na huduma za jamii wa Uturuki, Zehra Zümrüt Selçuk.

Mkutano huo wa tume ya pamoja baina ya Uturuki na Zambia umefanyika jijini Lusaka, Zambia. Selçuk, aliyekwenda mjini Lusaka, alikutana na wafanyabiashara mbalimbali raia wa Uturuki katika ubalozi wa Uturuki nchini humo.

Waziri Selçuk,  baadae alihudhuria mkutano wa kwanza a tume ya pamoja baina ya Uturuki na Zambia, tume ambayo ilianzishwa mwaka 2011.

Selçuk aliendesha mkutano huo kama mwenyekiti mwenza kwa kushirikiana na waziri wa mambo ya nje wa Zambia, Joseph Malanji. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mulungushi.

Selçuk alifahamisha kwamba mkutano huo wa kwanza wa tume ya pamoja utapelekea mahusiano ya kibiashara na uchumi baina ya mataifa haya mawili kuboreka zaidi.

" Mwaka 2003  ujazo wa kibiashara baina ya Uturuki na mataifa Afrika ulikuwa dola bilioni 5,4. Mwaka 2019 ujazo wa kibishara ulikuwa ni dola bilioni 25.3”.

Mawaziri hao wawili mara baada ya mkutano huo walisaini mikataba ya ushirikiano ambayo iliandaliwa kwa siku mbili na wajumbe wa pande zote mbili kwa pamoja.


Tagi: Zambia , Uturuki

Habari Zinazohusiana