Rais Erdoğan atolea wito mataifa ya Ulaya kuchukuwa hatua zinazostahili dhidi ya ugaidi

Recep Tayyıp Erdoğan atolea wito mataifa ya Ulaya kuchukuwa hatua zinazostahili katika mapambano dhidi ya ugaidi

Rais Erdoğan atolea wito mataifa ya Ulaya kuchukuwa hatua zinazostahili dhidi ya ugaidi


Recep Tayyıp Erdoğan atolea wito mataifa ya Ulaya kuchukuwa hatua zinazostahili katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Rais wa Uturuki atolea wito mataifa ya Magharibi kuchukuwa hatua zinazostahili katika mapambano dhidi ya ugaidi na kuheshimu kanuni.

Rais Erdoğan ameshirika katika hafla ilioandaliwa kwa ajili ya kuadhimisha miaka 100  tngu kuundwa kwa mji wa Kahramanmaraş.

Katika hotuba yake aliotoa katika hafla hiyo, rais Erdoğan amekemea bunge la  Ulaya  kuwapokea magaidi wa kundi la PKK, wakiwemo magaidi waliorodheshwa  katika orodha ya  magaidi wanaotafutwa na Uturuki.

Rais Erdoğan ametoa wito Umoja wa Ulaya kuwajibika ipasavya katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Kitendo cha bunge la Ulaya kuwakaribisha na kuzungumza na magaidi wa kundi la PKK ni wazi kuwa kuna  njama za undumila kuwili dhidi ya Uturuki amesema rais Erdoğan.
 Habari Zinazohusiana