Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Yeni Şafak: " Rais Erdoğan: iwapo mashambulizi ya jeshi la Syria yataendelea tutajibiza bila ya kujali makubaliano ya Sochi"

Rais wa Uturuki Recep Tyyıp Erdoğan  azungumza kuhusu mashambulizi dhidi ya jeshi lalake Idlib na kusema kuwa jeshi halitosita kujibu iwapo litashambuliwa na jeshi la Syria. Jeshi la Uturuki litajibu bila ya kujali makubaliano yaliosainiwa Sochi nchini Urusi.

Sabah: " Mazungumzo yasiokuwa ya kawaida Ankara"

Msemaji wa rais wa Uturuki Ibrahim Kalın  akutana na  muakilishi maalumu  wa Marekani Syria James Jeffrey . Katika mkutano wao  kulizungumiwa hali ya Idlib na mashambulizi yaliowalenga wanajeshi wa Uturuki. Kitendo hicho kimetajwa kuwa sio kitendo cha kuridhisha. Uwepo wa Uturuki Idlib ni kuhakikisha usalama wa raia katika eneo ambalo kulisainiwa makubaliano ya amani.

 

Habertürk: "  mwaka 2020  ni mwaka  "

Wizara ya utamaduni na utalii Uturuki amechagua mji wa Patar  katika kitongoji cha Kaş Antalya kuwa mji "lengo" la mwaka 2020. Inadaiwa kuwa mji huo uligunduliwa kuwepo karne kadhaa  huku pia ikitajwa kuwa karne 8 kabla ya Nabii Issa.Habari Zinazohusiana