Je wajua kwamba İstanbul ni moja kati ya miji ya kale zaidi duniani ?

Istanbul ni mji pekee duniani ambao ardhi yake ipo katika mabara 2 tofauti yaani bara la Ulaya na bara la Asia

Je wajua kwamba İstanbul ni moja kati ya miji ya kale zaidi duniani ?
1.jpg
d.jpg

Istanbul ni mji pekee duniani ambao ardhi yake ipo katika mabara 2 tofauti yaani bara la Ulaya na bara la Asia. Ni mji mkuu wa tamaduni mbalimbali kama Rumi , Ottomania, vile vile ni miongoni mwa miji ya kale zaidi duniani.

Istanbul ambao ni wenye idadi kubwa zaidi ya watu nchini Uturuki ni miongoni mwa miji mikubwa 5 yenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani. Mji huu una idadi kubwa ya watu zaidi ya nchi zenye idadi ya watu milioni 15 kama Ubelgiji, ugiriki, Tunisia, Ureno na nyingine nyingi. Hali hii sio ya miaka ya hivi karibuni pekee,kwani miaka ya 1500 Istanbul ulikuwa ni miongoni mwa miji yenye idadi ya watu wengi zaidi duniani. Istanbul pia ni miongoni mwa miji ya kitalii inayokuwa kwa kasi zaidi pamoja  na kuwa miongoni mwa miji ya kibiashara inayokuwa kwa kasi zaidi.

Kuna ngano za kale nyingi kuhusiana na mji wa Istanbul. Moja wapo ni kuhusiana na lango la Istanbul...

Kwa mujibu wa simulizi chini ya lango la Istanbul kuna hazina kubwa ya dhahabu na kuna kipindi Wajapan walitaka  kusafisha bure, lango hilo ili wajipatie hazina hiyo. Miaka ya 1950 ulifanyika uhamiaji mkubwa kwatika Istanbul. Usemi wa kwamba jiwe la Istanbul ni dhahabu, inawezekana imetokana na ngano iliyotajwa hapo juu.Habari Zinazohusiana