Je wajua kwamba Uturuki inaongoza kwa utajiri wa mimea ya asili duniani ?

Nchini Uturuki kunamea mimea ya asili zaidi ya elfu 11 miongoni mwa mimea hiyo elfu 3 asili yake ni Uturuki

Je wajua kwamba Uturuki inaongoza kwa utajiri wa mimea ya asili  duniani ?

Mimea ipatayo elfu 11 humea nchini Uturuki. Miongoni mwa mimea hiyo aina elfu 3 asili yake ni Uturuki. Hili linaifanya Uturuki kuwa nchi ambayo ina mimea mingi zaidi ya asili barani Ulaya.

Utajiri huu wa uoto wa asili nchini Uturuki unatokana na kuwepo kwa maeneo ya kijiografia ya aina tofauti ikiwemo milima, vilevile hali ya hewa tofauti, ikiwa ni nchi inayounganisha mabara tofauti.

Siku hizi Uturuki huuza nje mimea ya asili ya aina tofauti ambayo hutumika katika tiba na kutoa harufu nzuri. Mimea hii ambayo kwa karne nyingi imekuwa ikimea katika ardhi yenye rutba ya Anatolia imesambazwa duniani. Miongoni mwa vyakula vinavyotokana na mimea yenye asili ya Anatolia ni kma vile cheri, lozi, embe ulaya , ngano, chickpeas, kunde, tini. Miongoni mwa mauwa yenye asili ya Anatolia  yaliyosambazwa duniani ni pamoja na “tulip”, “snowdrop” na “Colchicum”.


Tagi: mimea , Uturuki

Habari Zinazohusiana