Çavuşoğlu; "Kuuawa kwa Suleiman kumuieweka amani ya kanda yetu katika hatari kubwa"

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Çavuşoğlu amesema Kuuawa kwa jenerali Suleiman kumuieweka amani ya kanda katika hatari kubwa

Çavuşoğlu; "Kuuawa kwa Suleiman kumuieweka amani ya kanda yetu katika hatari kubwa"

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu, amesema shambulizi la Marekani lililopelekea kuuawa kwa mkuu wajeshi la ulinzi wa mapinduzi raia wa Iran, jenerali Kasim Suleiman kumeiweka kanda katika hatari kubwa ya kupoteza utulivu.

Çavuşoğlu alifahamisha kuwa Uturuki inafanya juhudi kubwa katika kujaribu kutatua tatizo lililopo au kupunguza mvutano. Katika muktadha huo Rais Erdoğan  wa Uturuki amefanya mawasilino na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Rais wa Iran Hasan Ruhani, Rais wa Irak Berhem Salih  na amir wa Qatar Sheyh Tamim bin Hamad Al Sani.viongozi wengine aliofanya nao mazungumzo ni  pamoja na waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Kansela wa Ujerumani bi Angela Merkel.

Çavuşoğlu alisema,

 " Ili kutatua tatizo lililopo au ili kupunguza mvutano, katika siku zinazokuja tutaendelea kufanya mazungumzo na nchi nyingine. Kama mjuavyo Alhamis ijayo Rais wa Urusi, Vladmir Putin atakuwa ziarani jijini Istanbul.  Rais wetu atazungumza na Putin juu ya suala hili uso kwa uso. Haswa wasiwasi wetu mkubwa ni Irak na mataifa mengine yasigeuzwe uwanja wa mapambano. Kwani hilo ni hatari kubwa kwa Irak na kanda nzima kwa ujumla.Mazungumzo yetu na Irak pia yanaendelea. Hivyo basi ili kupunguza hatari iliyopo Uturuki itaendelea kufanya kila liwezekanalo”.Habari Zinazohusiana