Gari la kituruki lawa gumzo kila kona duniani

Latazamiwa kutoa ushindani mkali kwa gari la umeme la kimarekani Tesla

Gari la kituruki lawa gumzo kila kona duniani

Gari jipya la kituruki lawa gumzo dunia nzima…

Gari jipya la kituruki la kwanza la aina yake lililobuniwa na kutengenezwa Uturuki kwa asilimia 100, jana lilitambulishwa rasmi kwa ulimwengu. Utambulisho huo ulifanyika katika mji wa Gebze huko Kocaeli. Mara baada ya kutambulishwa gari hilo limekuwa ndio gumzo katika mitandao ya kijamii.

Katika ulimwengu wa mitandao ya kijamii dunia nzima gari la kituruki imekuwa ndio habari namba moja,huku tag #Yerlioto ikia ndio gumzo.

Ndani ya muda mfupi kulikuwa na “tweets” zaidi ya laki moja kuhusiana na gari la kituruki.

Shirika la habari la Reuters liliiandika habari ya gari la kituruki kwa kichwa cha habari “Uturuki yatambulisha gari lake kwanza”.

Gazeti la Daily Mail la Uingereza liliandika Gari la Kituruki kutoa ushindani kwa gari la umeme la kimarekani la Tesla.

Gazete,  liliandika “Rais  Erdoğan, atambulisha gari la mfano la TOGG linalotazamiwa kutoa ushindani kwa  Tesla".

Habari kutoka Bloomberg ilisema "Uturuki yatambulisha mradi wa magari ya kituruki wa kwanza wa aina yake wenye thamani ya dola bilioni 3,7 ”

Al Jazeera iliandika " Uturuki yatambulisha gari lake la kwanza”.

Rais Erdoğan alisema magari ya Uturuki siyo kwa ajili ya soko la ndani pekee bali ni kwa ajili ya dunia nzima ukianzia na nchi za Ulaya.

 Habari Zinazohusiana