Mapishi ya Kituruki
Supu ya bibi harusi

Supu ni muhimu sana katika vyakula vya Kituruki. Bila kujali msimu, ni tabia ya kawaida kwa waturuki kuanza mlo wowote na supu. Bila ya kujalisha tajiri au maskini,vijijini mijini, bila kujali tofauti katika jamii,supu ni muhimu. Supu kwa kawaida hunywewa wakati wa chakula cha mchana au jioni.
Kuanza siku na supu kifungua kinywa ni tabia ya kawaida, haswa vijijini. Leo, tutakupa maelekezo ya jinsi ya kutengeneza supu nzuri kabisa na maarufu Anatolia.
. Jina la supu yetu ni supu ya “Ezo Gelin”ikimaanisha “bibi harusi Ezo”.Jina hili la mwanamke linaaminika kutokea katika mji wa Gaziantep nchini Uturuki.Tutizame inavyotengenezwa.
MAHITAJI;
Kikombe 1 ½ cha dengu nyekundu
Vijiko 3 vya mchele
Vijiko 2 bulgur
Kitunguu 1
Kijiko 1 cha nyanya
Kijiko 1 cha siagi
Vikombe 6 vya maji ya moto
Kijiko 1 cha mint
Kijiko 1 cha chumvi
1/2 kipande cha maji ya limao
Kijiko 1 cha pilipili nyekundu
JINSI YA KUTENGENEZA
Ni wakati wa kupika supu ya "bibi harusi". Kwanza, suuza dengu yako vizuri mpaka maji meupe yaishe.. Chemsha maji yamoto kwenye sufuria kubwa. Osha na kumwaga dengu nyekundu ndani ya sufuria. Ongeza vijiko 3 vya mchele, vijiko 2 vya bulgur na kijiko 1 cha chumvi. Pika kwa muda wa dakika 35 hadi dengu nyekundu iwe laini. Yeyeyusha kijiko 1 cha siagi katika sufuria tofauti. Ongeza kitunguu 1 na uanze kukaanga. Ongeza kijiko 1 cha nyanya iliyosagwa au nyanya ya kopo kisha ongeza kijiko 1 cha mint.Endelea kukaanga kwa dakika 2 zaidi. Epua mchuzi wako. Chemsha dengu kwenye sufuria, ongeza mchanganyiko wako wa nyanya na vitunguu. Kisha pika supu kwa dakika 10.
Supu yako ipo tayari.Hunywewa ikiwa ya moto kwa kunyunyizia limao na pilipili nyekundu.