Kombora la Bozdoğan lapita majaribio ya kwanza
Uturuki inakuwa ni miongoni mwa mataifa 9 duniani yenye uwezo wa kuzalisha kombora la aina hii linalotoka anga moja hadi jingine

Bozdoğan, kombora la kwanza la kituruki linaloeweza kurushwa toka anga moja kwenda jingine limefanyiwa majaribio ya kwanza kwa mafanikio.
Wizara ya viwanda na teknolojia imetoa taarifa kuhusiana na kombora hilo lililotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya kituruki.
Katika taarifa hilo ilifahamishwa kwamba Bozdoğan, kombora ambalo limetumia gharama kubwa kutengenezwa hivi sasa limekamilika na hivi karibuni litapachikwa katika ndege vita haribifu zinazotengenezwa nchini Uturuki aina ya F-16.
Kwa mafanikio hayo Uturuki inaingia katika kundi la 9 duniani zinazoweza kutengeneza makombora ya aina hii