Kahawa ya Kituruki

Kahawa maarufu ulimwenguni,"Turkish Coffee"

Kahawa ya Kituruki

Je! Unapenda kahawa? Kuamka asubuhi na ampema na kupata kikombe kimoja cha kahawa.Nadhani ni raha sana.

 

... Kwa hali yoyote, vikombe vya kahawa bilioni 2.25 hunywewa wa kila siku ulimwenguni. Kahawa ya Kituruki ni kati ya kahawa mabazo hutumiwa kwa kiasi kikubwa duniani.

 

Kahawa ya Kituruki ni tofauti kabisa kuanzia inavyopikwa mpaka inavyonywewa.

Na hata baada ya kunywewa kahawa ya Uturuki bado ina umuhimu kwani kuna baadhi ya watu maalumu wanaweza kusoma machicha ya kahawa yaliyobaki chini ya kikombe yana maana gani katika maisha yako.Mustakabadhi wa maisha yako unaweza kuonekana katika vichicha hivyo vya kahawa nchini Uturuki.

 

 Licha ya kuwa kahawa hiyo huitwa kahawa ya Uturuki,hakuna uwezekano hata kidogo kwa ardhi ya Uturuki kulima kahawa.

 

Ukweli ni kwamba kahawa hii inaitwa kahawa ya Kituruki kutokana na njia tofauti za kupikia zilizovumbuliwa na Waturuki. Kwa mara ya kwanza, kahawa ilipelekwa Anatolia kutoka Yemen katika karne ya 16. Ilipendwa na kuenezwa ndani ya muda mfupi

 

Shukrani kwa Waturuki, kwamba ulimwengu wa magharibi nao ukapata kuijua kahawa.

Wafanyabiashara wa Kiveneti walioenda  Uturuki wakati wa karne ya 17 enzi za Ottoman,waliiona kahawa,wakaionja,wakaipenda na kisha wakaichukua Ulaya.

 

Kahawa hiyo, ambayo hapo awali ilikuwa ikiuzwa barabarani, ilianza kuuzwa kwa mara ya kwanza mnamo 1645 katika duka nchini Italia, yani kwenye “cafe”. Kuanzia miaka ya kwanza ya karne ya 18, kahawa ilienea sana barani Ulaya. Hadithi ya kuingia kahawa nchini Austria pia ni ya kufurahisha sana. Jeshi la Ottoman, ambalo lilizingira Vienna mnamo 1683, baadaye wakati wa kuondoka liliacha nyumamagunia ya kahawa .Kwanza Waaustria walidhani ya kwamba kahawa iliyokuwa ndani ya magunia ilikuwa ni chakula cha wanyama.

Georg Kolschitzky, ambaye aliwajua Waotomani, alitaka apewe magunia hayo na kuyafanya kuwa mtaji na akafungua mahali pa kunywa kahawa huko Vienna. Hivyo ndivyo wananchi wa nchi hiyo walivyoijua kahawa.

 

Kahawa ya Kituruki, iliyoandaliwa na kusambawa kwa njia hiyo hiyo tangu karne ya 16, ina nafasi maalum katika tamaduni ya Kituruki. Kahawa ni moja ya njia muhimu zaidi ya ujamaa, inawaleta watu kutoka ngazi zote za jamii pamoja.. Kikombe cha kahawa wakati mwingine huashiria mazungumzo mazuri, wakati mwingine wasiwasi wa pamoja, na wakati mwingine habari juu ya siku zijazo. Kivipi?.

Katika mila ya kawaida, baada ya kunywa kahawa, kikombe huchukuliwa na kuwekwa pembeni.Kwa Waturuki kikombe hicho huwekwa pembeni kwa kugeuzwa juu chini na huachwa mpaka kikauke.Mtu huomba kile anachotaka moyoni na kisha kikombe hugeuzwa na kutizamwa majani yaliyoganda yanaashiria nini kwa mtu aliyemaliza kunywa kahawa hiyo.Kuna wataalamu wenye uwezo wa kusoma siku za usoni zam tu huyo.

 

Baada ya historia hiyo fupi,sasa tutizame jinsi kahawa ya kituruki inavyotengenezwa.

 

MAHITAJI;

Kijiko 1 cha kahawa iliyotiwa unga (ikiwa unaweza kupata iliyo tayari kutumia.)

-1 Kikombe(kahawa) cha maji

- sukari (1/3 hadi kijiko 1)

 

Utayarishaji wa kahawa ya Kituruki ni kama ifuatavyo;

Kwanza, ikiwa huna tayari kahawa iliyosagwa kwanza isage mpaka upatikane unga mzuri.

Halafu kahawa hupikwa kwenye chombo maalum cha kuoka kahawa. Ikiwa hauna sufuria ya kahawa, basi tumia sufuria ya kawaida au chombo cha kuchemshia maziwa.Weka maji baridi na sukari kwenye kahawa. Hapa inafaa kutoa maelezo ya kina juu ya mada ya sukari. Kwa sababu sukari ya kahawa ya Kituruki huwekwa wakatş wa kupika,  baada ya kupika, sukari na maziwa kamwe haviongezwi tena!.

 Kahawa imegawanywa katika makundi nne kulingana na sukari iliyoongezwa; kahawa bila ya sukari, kahawa yenye sukari kidogo ,kahawa yenye sukari ya kati na kahawa yenye sukari.

Hakuna sukari inayoongezwa kwenye kahawa ya kawaida (Black Cofee)

Unapaswa kuweka kijiko kidogo 1/3 cha sukari kwa kahawa ya sukari kidogo,kijiko 2/3 kwa kahawa ya sukari ya kati na kijiko 1 au zaidi kwa kahawa iliyo na sukari.

Sasa, tuendelee kupika kahawa yetu; Kahawa, sukari na maji yaliyowekwa ndani ya sufuria huchanganywa vizuri na kuwekwa kwenye jiko. Weka moto wa chini, pika kwa muda wa dakika 3-4 hadi povu lionekane.Mwaga povu hilo katika kikombe cha kahawa kwani povu huashiria kahawa bora.Povu likiwa jingi na kahawa inakua nzuri.

Baada ya kumwaga povu rudisha kahawa kwenye moto na usubiri ichemke.Ikichemka mwaga kwenye kikombe chako ulichokuwa umemwaga povu lako tayari.

Kwa wale wapendao maziwa,wanaweza kuongeza maziwa wakati wa kupika kahawa yao.

Kahawa yako ipo tayari.Waweza kunywea maji na dessert pembeni.

Furahia kahawa yako!.Habari Zinazohusiana