Familia ya Mohammed Morsi yatoa shukrani kwa rais Erdoğan

Familia ya aleikuwa rais wa Misri Mohammed Morsi yatoa shukrani kwa rais wa Uturuki

Familia ya Mohammed Morsi yatoa shukrani kwa rais Erdoğan

 

Familia ya aleikuwa rais wa Misri Mohammed Morsi aliefariki akiwa mahakamani imetoa shukrani kwa rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan.

Shukrani hizo zimetolewa na familia ya Morsi kwa kusema kuwa rais Erdoğan hakuwaachape katika upwekwe katika kipindi chote ambacho rais Morsi alikuwa  amezuiliwa hadi kufariki kwake akiwa mahakamani.

Katika kituo cha runinga cha Al Jazeera mtoto wa Mohammed Morsi Abdullah Morsi amesema kuwa serikali ya Misri haikuruhusu kutolewa kwa salama za rambi rambi kwa wanafamilia baada ya kifo cha baba yake na kukumbusha kuwa sala ya jejnza  kwa ajili yake iliandaliwa katika msikiti wa Al Aqsa.

Mamilioni ya waumini ulimwenguni kote walidiriki sala ya jeneza kwa ajili ya Mohammed Morsi.

Katika mahojiano katika kituo hicho cha habari, Abdullah Morsi amesema kuwa katika historia tuko kama hilo lilikuwa bado halijarokea.

Shukrani za dhati zilitolewa pia kwa amir wa Qatar Sheikh Tamim Bin Hamed al Thani, serikali ya Maleisia na kwa rais wa zamani wa Tunisia Monsef Mazouki.Habari Zinazohusiana