Je Wajua?

Historia ya "Turkish Delight"

Je  Wajua?

Je, unajua kwamba vyakula vitamu vya kituruki haswa “lokum” ni maarufu ulimwenguni, Napoleon, Winston Churcill na Picasso ni miongoni mwa watu maarufu ambao walipenda dessert hii ya Kituruki?

Ni dessert ya kitamaduni ya Kituruki iliyotengenezwa kwa kutumia , maji, sukari na wanga. Ingawa inajulikana katika Anatolia tangu karne ya 15, lokum, ambayo ilienea katika Dola ya Ottoman katika karne ya 17, ilianza kutambuliwa Ulaya katika karne ya 18 kwa jina la 'Turkish Delight' kupitia msafiri wa Uingereza. Ladha yake ya matunda na asali ilibadilishwa karne ya 17 na kuanza kutumia sukari inayojulikana kwa jina “sukari ya kelle”.

Viongozi wengi ulimwenguni kama Winston Churcill na Napoleon walipenda sana dessert hii, na mchoraji Picasso alipenda kula wakati akichora  kama njia ya kumpa  motisha zaidi.

Hivi leo kuna lokum za aina tofauti.Kuna lokum isiyochanganywa na kitu na nyingine huchanganywa na hazelnut, pistachio, walnut, almond, nazi, machungwa, jan la uwaridi, strawberry, limao, mint, vanilla, tangawizi na aina nyingine nyingi.Habari Zinazohusiana