Mji wa Istanbul wazipita nchi 131 kwa idadi ya watu

Asilimia 18.4 ya watu nchini Uturuki wanaishi Istanbul, Jiji hilo lina wakaazi wapatao milioni 15 elfu 67 na 724

Mji wa Istanbul wazipita nchi 131 kwa idadi ya watu

 

Istanbul ni mji wenye idadi kubwa ya watu kupita miji yote ya Uturuki. Idadi ya watu jijini Istanbul imefikia  milioni 15 elfu 67 na 724. Kwa idadi hiyo Istanbul inakuwa ina idadi ya watu wengi kuzidi nchi 131.

Shirika la takwimu la Uturuki kwa kushirikiana na fuko la Umoja wa mataifa la idadi ya watu (UNFPA) wametoa takwimu ambazo zinaonyesha mnamo mwaka 2018 Uturuki ilikuwa na idadi ya watu wapatao milioni 82 elfu 3 na 882. Asimilia 18.4 ya watu Uturuki wanaishi Istanbul.

Idadi ya watu jijini  Istanbul imeongezeka kwa  watu 907,257  ndani ya miaka 5. Katika kipindi hicho mji wa Istanbul ambao ndio unaoongoza kwa idadi ya watu katika miji ya Uturuki uliziacha nyuma nchi 131 kati ya nchi 204.

Mji wa Istanbul una Idadi kubwa ya watu  kupita nchi kama Ubelgiji ( idadi ya watu milioni 11.5), Ugiriki ( idadi ya watu milioni 11.1), Austaralia ( idadi ya watu milioni 8.8), Uswizi ( idadi ya watu milioni 8.5) na Bulgaria ( idadi ya watu milioni 7).Habari Zinazohusiana