Waziri wa ulinzi wa Uturuki na mapambano dhidi ya ugaidi

waziri wa ulinzi wa Uturuki athibitisha  malengo ya Uturuki katika mapmabano yake dhidi ya ugaidi

1135668
Waziri wa ulinzi wa Uturuki na mapambano dhidi ya ugaidi

Hulusi Akar, waziri wa ulinzi wa Uturuki athibitisha  malengo ya Uturuki katika mapmabano yake dhidi ya ugaidi.

Waziri wa ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar amesema kuwa jeshi la Uturuki limemaliza mataarisho yake  na kuwa ala kamili  kuanza operesheni dhidi ya magaidi ambao wameweka ngome zao Mashariki mwa Frati.

Magaidi waliweka ngome zao Manbiji ndio lengo la operesheni ya jeshi la Uturuki amesema Hulusi Akar.

Hayo waziri wa ulinzi wa Uturuki ameyazungumza  katika  ziara aliofanya mkoani Eskişehir Jumanne.

Hulusi Akar amesema kwamba  jeshi la Uturuki lipa tayari kwa wakati wowote kuanza na operesheni yake Manbij dhidi ya magaidi kinyume na inavyodaiwa na baadhi ya watu kwa kupandikiza chuki na ugawanyika kwa kunesha tofauti kati ya  jamii ya wakurdi na waarabu.

Lengo la operesheni ya jeshi la Uturuki Manbij ni kuwaondoa magaidi Mashariki mwa Frati.

Akar ametoa pongezi kwa jeshi  baada ya operesheni iliopelekea magaid kuondolea Afrine na maeneo mengine Kaskazini mwa Syria.

Katika hafla hiyo mkoani Eskişehir, Akar amesema kuwa  Uturuki haina tatizo la aina yeyote na jamii ya wakurdi bali magaidi  wanaoyumbisha usalama katika ukanda.Habari Zinazohusiana