Sekta ya utalii yavunja rekodi Uturuki

Waziri wa utalii wa Uturuki Numan Kurtulmuş ameisifu sekta ya utalii nchini humo.

Sekta ya utalii yavunja rekodi Uturuki

Waziri wa utalii wa Uturuki Numan Kurtulmuş ameisifu sekta ya utalii nchini humo.

Sekta ya utalii imevunja rekodi mwaka huu ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Ripoti zimeonyesha kuwa watalii milioni 11.8 wametembelea nchini humo ndani ya miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2018.

"Takwimu hizi ni bora kuliko wakati wote. Nawapongeza, pia ongezeko la asilimia 30.8 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Jambo hili ni muhimu kwa Uturuki, kwa kweli ni jambo la kujivunia",alisema waziri Kurtulmuş.

Mapato ya utalii yamefikia dola bilioni 32 kwa watalii milioni 40.

 


Tagi: Utalii , Uturuki

Habari Zinazohusiana