Mtazamo

Februari 28: Mapinduzi ya mwisho ya Vita Baridi

Mtazamo

Kutoka chuo kikuu cha Ankara Yildirim Beyazit kitengo cha Sayansi za Siasa Dr.Kudret BÜLBÜL anafanya tathmini ya mada yetu ya leo

Februari 28: Mapinduzi ya mwisho ya Vita Baridi

Miaka 21 iliyopita, tarehe 28 Februari 1997 ni siku iliyotokea moja ya mapinduzi muhimu ya kijeshi katika historia ya Uturuki ya hivi karibuni.

Mapinduzi ya kijeshi au majaribio ya mapinduzi ya kijeshi si jambo geni kwa historia ya Uturuki. Uturuki imekuwa ikikabiliwa na hatua kama hizo karibu katika kila muongo: 1960, 1971, 1980, 1997 (Februari 28) 2007 (Aprili 27), 2016 (Julai 15)

Tukitizama mapinduzi ya mwaka wa 1997, tunaweza kudhani kuwa ilichukua muda kwa mapinduzi mapya kufanyika baada ya yale ya mwaka 1980. Lakini hali inaweza kueleweka baada ya kujua kuwa mkuu wa maandamano Jenerali Evren aliachishwa madaraka kwa muda wa miaka minane.

Kwanini Uturuki inakuwa inakabiliwa na mapinduzi kila muongo?

Ukiangalia kesi ya Uturuki, nchi za kimataifa zinajua kuwa nchi kama Uturuki zikiachiwa kuendelea kama kawaida basi zinaweza kufanya mambo makubwa. Kutokana na hili, ni muhimu kuweka nchi hizo chini ya udhibiti mara kwa mara. Tumejifunza hili kutoka Ujerumani ambapo mara mbili wamekuwa wakitaka kubadilisha utaratibu wa kimataifa na hivyo basi katiba ikalazimishwa na vilevile nguvu ya jeshi na silaha vikadhibitiwa.

 Uturuki pia imeshuhudia jambo hili kwa mara nyingine wakati wa miaka ya Waziri Mkuu Adnan Menderes, ambaye aliuawa katika mapinduzi ya kijeshi. Kwa sababu hii, mfumo wa kutetea ulianzishwa ili kuwaweka wapiga kura chini ya udhibiti na Katiba ya 1961. Mapinduzi yanayojaribiwa kila muongo ni njia za kuweka wananchi chini ya udhibiti.

Athari zinazoachwa katika nchi kama Uturuki,zinaweza kujieleza ukitizama mambo yake ya ndani.Wiki iliyopita, mkuu wa zamani wa CIA, James Woolsey, katika uchunguzi uliofanywa na Mwendesha Mashitaka Robert Mueller kuhusu suala la Urusi kuingilia katika uchaguzi wa Marekani, alikiri kwamba Marekani huingilia katika uchaguzi wa nchi nyingine pia. Vile vile, baada ya mapinduzi ya mwaka 1980 nchini Uturuki, Mshauri wa taifa la Marekani katika  Baraza la Usalama  Paul Henze, wakati wa utawala wa rais wa Marekani Jimmy Carter alisema kuwa “watoto wetu wamefanikiwa”.

Mwishoni mwa 1990  Rais Özal aliuawa pamoja na kuwa alileta  maendeleo ya kiuchumi na uhuru katika taifa lake. Baadaye, wakati wa Refah Yol, uchumi wa nchi ulikuwa kwa  kasi chini ya uongozi wa marehemu waziri mkuu Erbakan. Muenendo ukiendelea hivi basi Uturuki inaweza kushindwa kudhibitiwa na hivyo kujitengenezea njia yake yenyewe. Hapa ni mapinduzi ya Februari 28 katika mazingira kama hayo.

Mchakato wa Februari 28

Mchakato huo ulianza Februari 28 wakati mizinga ilipofyatuliwa kutoka katikati ya jiji la Wilaya ya Sincan ya Ankara. Jambo hili linaweza kuonekana la kawaida sana lakini wakati wa siku za nyuma suala la bunge  kuzungukwa na  mizinga ambapo tayari nchi hiyo mlishaishi ambapo mawaziri wakuu waliuwa,akili yako inakuwa tayari imeshaathiriwa.

Mchakato huo uliendelea. Katika Baraza la Usalama la Taifa, harakati zilikuwa tayari zimeanza kuchukuliwa ambapo idadi ya askari na wapiganaji iliikuwa sawa na ile ya raia wa kawaida. Baada ya mashambulizi ya askari kutoka nje, nchi nzima ilikuwa imefungwa. Nchi iliingia mchakato na harakati ambazo ziliwahi kufanywa hapo awali. Waamuzi, watendaji wa serikali, NGOs walianza kujadili ni hatari gani nchi ilikuwa nayo.

Matokeo

Lakini mchakato haukuishia hapo kwani kulikuwa na kuipindua serikali, miaka ya kutokuwa na msimamo ,watu kuwekwa  kizuizini, watu wengi kufukuzwa kazi, vifo, vijana kujiua na vilevile athari kwa vizazi vijavyo

Haki za msingi na mafaniki yote ya nyuma yaliyopatikana yakachukuliwa na utawala wa kijeshi ukarudi nchini Uturuki. Kama ilivyoonekana mwaka 2002, uchumi wa nchi ulianguka.

Ikawa ni  kesi ya rushwa, uibizi na uharibifu wa mashtaka ...

Na Baadaye

Feb 28, Uturuki ambayo ilitaka kuwekwa  chini ya udhibiti wa ndani na nje ya majeshi ilimalizika baada ya matokeo ya vita baridi.Baada ya vita hizo ilionekana kuwa Uturuki haiwezi kudhibitiwa ten ana ikaanza kuwa na utandawazi na zam aza mawasiliano,vyama vingi,tamaduni,na demokrasia.Tukuiangalia miaka ya nyuma hatuwezi kusema kuwa 28 Februari ilikuwa na mafanikio kutokana na vita baridi lakini mafaniki yake yanaweza kuonekana katika masuala mengine kama vile kuleta amani na mafanikio katika nchi.Kwa sababu wakati huo makundi ya kiraia na ya kidini ambayo kwa sasa ni

Kundi la FETÖ yaliisha.

Kwahiyo 28 Februari na 15 Julai ni kati ya tarehe zilizofanya mabadiliko mengi katika nchi ya  Uturuki.Uongozi wa rais Reccep Tayyip Erdoğan na wa ustwi wa kitaifa haukujisalimisha .Jula 15 watu wengi walipoteza maisha.Tuu 250 huku wengine zaidi ya 2000 wakiwa wamejeruhiwa.Lakini tulihakikisha tunaiokoa nchi yet una vizazi vya baadaye.

Mapinduzi ya nchi nzima yamefundisha ulimwengu wote jinsi ya kuyabadilisha kwa namna ya kidemokrasia.

Mafunzo ya tarehe 28 Februari

Ni wazi kuwa watendaji wa kimataifa hufanya mambo kwa maslahi yao wenyewe.Wanapotaka kuidhibiti nchi hutumia njia zote bila kujali atahri zinazoweza kuleta kwa taifa husika.Hawajali haki za binadamu wala demokrasia. Kwa watendaji wa kimataifa, haijalishi kama hatua hii ina uhalali wa kijeshi, wa kidini, wa kidunia au wa kitaifa.Kuzuia mfumo wa uhifadhi ni kufungua maeneo yote ya mfumo iwezekanavyo. Ni mojawapo ya vipengele muhimu zaidi vinavyozuia utaifa na siasa,Kwahiyo ni muhimu kwa mataifa yote yanayotaka kuishi kwa heshima na kutopoteza hadh yake kulitambua hilo.

Kutoka chuo kikuu cha Ankara Yildirim Beyazit kitengo cha sayansi za Siasa Profesa Dr. Kudret BÜLBÜL alipendekeza tathmini ya suala hilo ...

 Habari Zinazohusiana