Mji mkuu wa Utamaduni wa Istanbul

Mji mkuu wa Utamaduni wa Istanbul

356443
Mji mkuu wa Utamaduni wa Istanbul

Mji wa Istanbul uliokuwa mji mkuu wa Utamaduni mwaka 2010, una sifa nyingi za kuwa mji wa kiutamaduni. Mji huu unasifa zote za kisasa na kimila. Tunaposema mji wa Istanbul ni mji mkuu wa Utamaduni, tunaangalia mtazamo wake,rangi yake,na hata harufu yake nzuri inayotokana na maua yaliyosheheni katika mji huo. Katika kipindi chetu cha leo tukakupelekea katika mahali penye historia nzuri katika jiji hili la Istanbul.

"Sauti ya Istanbul" unaposikia neno hili moja kwa moja tunafikiria ni sauti za sala zinazotoka katika minara ya misikiti ya Istanbul, sauti za matangazo ya wafanyabiashara wapitao kwa magari mitaani, kilio cha sauti za ndege, sauti za filimbi ya meli, kelele za barabarani, na sauti za muziki. Haya yote ni maisha ya kawaida kukutana nayo katika jiji hili la Istanbul, lakini sauti ya Istanbul, haiwezi kujitosheleza yenyewe.kwa muda mrefu kumekuwa na sauti nyinine zinazokaribia jiji hili. Kwa mfano, tafsiri ya wanamziki maarufu wa jazz. Pengine, unaweza kufikiria jazz inaweza kusikilizwa katika ukumbi au kutazamwa katika ukumbi hewa wa maonesho.Hata hivyo, jazz imeweza kutikisa katika matukio ya kimataifa mjini Istanbul,mziki wa jazz unaweza kusikia karibu kila kona ya jiji hilo.

Maonesho ya kimataifa ya muziki wa jazz kwa muda wa miaka 16, maelfu ya watu wamekuwa wakijaza masikio yao kwa muziki huu wa jazz . Mwaka huu maonesho ya muziki wa jazz yamefanyika tarehe 15 za mwanzo wa mwezi wa 7,wanamuziki maarufu watatumbuiza katika jukwaa la maonesho hayo. Tamasha hilo la jazz litafanyika tena jijini ifikapo tarehe 30. waandaaji wa tamasha hilo Wizara ya Utamaduni na Sanaa,wamewaalika wapiga gitaa maarufu duniani Stanley Clarke, Marcus Miller na Victor Wooten, kuwa wageni rasmi. Lakini tukumbuke kuwa hatupo hapa kuwaelezea kuhusiana na Tamasha, hapana tungependa kukuelezea kuhusiana na muziki wa jazz,je,umeeneaje katika jiji hili,na pia kuangalia maeneo muziki wa jazz ulipotawala.

Fikiria manzari ya waimbaji jazz wakitumbuiza katika boti huku ndege wakipaa angani. Mji huu ni moja ya njia za ndege wakiwa wanahama hama.Baris Manco mwanamuzi maarufu aliyefariki miaka 10 iliyopita.mwanamuziki Mancoalieneza sana muziki wa jazz kipindi cha uhai wake.kwa sababu kila tamasha lililofanyika alishiriki katika muziki wa jazz katika matasha ya ukumbini na hata ya uwanjani,isitoshe alitumbuiza muziki katika nyumba za muziki wa usiki,katika makutano,katika majumba ya makumbusho na hata katika mitaa. Moja ya vipengele vikuu vya muziki huu wa jazz ilikuwa katika mashua, mwaka huu jazz inatarajiwa kutumbuizwa katika meli ya Balkani. Sauti ya muziki wa jazz utapata kuvutia watu wengi na hata viumbe wa majini, muziki huu utapata kusikika katika majumba na hata Ikulu na watu wengi watapata kuburudisha mioyo yao. Wapenzi wa muziki kutoka mabara yote mawili la Asia na Ulaya wanashauku kubwa ya kusikia muziki huu.

Pasi na maeneo ya Boti na maeneo atika mitaani, muziki wa jazz ulikuwa ukitumbuizwa katika maeneo maalum sana ya kijadi. Moja ya maeneo haya ni katika jengo la makumbusho la Hagia Eirene. Tungependa kuwatambulisha jengo hili ambalo pia ni moja ya eneo lenye ufanyaji wa shughuli nyingi.

Nyumba hii ilijengwa na mfalme Constantine wa Byzantine , wakati alipokuwa katika heka heka za kuanzisha tena wa mji huu, kanisa la St Irene ilijengwa katika nyumba ya Warumi katika miaka ya 330. Kwa mujibu wa vyanzo vya kale, miundo ya ujenzi wa Kirumi kama vile, Artemi, Aphrodite na Apollo ilinufaika na hekalu za magofu hayo. Maana ya Aya Irini katika kamusi ni “Amani takatifu”. Hiyo ilikuwa ni maana, lakini Irene, wakati wa enzi hizo, lilikuwa ni jina takatifu la mtu aliyeishi katika karne hizo. . Kwa mujibu wa maelezo hayo Penelope ni jina la binti aliyekuwa akifanya matukio mbalimbali ya kueneza dini ya Ukristo.Ingawa hawakuweza kuuawa na wapagani.wapagani hao walishuhudia miujiza mingi na mwishowe walibadili dini na kuwa wakristo. Mji ukawa na amani na maelewano. .Aidha dini ya kristo ndo dini ya kwanza kujulikana katika eneo hilo na jumba la kanisa hilo kupewa jina la Hagia Eirene.

Sifa za kipekee za makanisa zilizokuwepo mpaka wa leo zilitokea kwa wa Bizansi, kanisa la Atiria ni kanisa pekee lilibakia . Atiria, ni kanisa lenye miundo ya ujenzi wa kirumi. Kanisa hilo limejengwa kwa kutumia mbao.
Kanisa la Hagia Irene, lilichomwa moto wakati wa vita katika miaka ya 532. na lilijengwa upya na mfalme Justinian. Atrium ilichomwa moto mwaka 564 kwa mara nyingine tena, jengo hilo lilipitiwa na tetemeko mara nyingi. Kila uhariboifu uliolipata jengo hilo lakini bado liliweza kudumu mpaka wa leo. Hapakuwa na mabadiliko makubwa ya ujenzi wa jengo hilo kama ilivyokuwa katika kipindi cha Ottoman ilipoikomboa jiji la Istanbul.
Katika kipindi cha Ottoman , Hagia Eirene, lilitumika kama nyumba la kuhifadhia akiba za silaha katika karne ya 19, Kanisa hilo liliandaliwa kuwa makumbusho ya kwanza ya Dola ya Ottoman. Na kupewa jina la Muze-i Humayun yaani makumbusho ya dola.
Jengo hilo la Makumbusho lilikuwa likitumiwa ktika ukusanyaji na uhifadhi wa mambo ya kale na silaha za zamani, lakini mwaka 1908 jengo hilo likagawanywa katika sehemu mbili, na pia kuwa jengo la makumbusho ya kijeshi. Jumba hilo lilibakia hivyo kwa miaka mingi jengo la makumbusho la Hagia Irene, kwa sasa linajulikana kama jengo la makumbusho la Hagia Sophia.

Jengo hili la makumbusho lilikuwepo kwa muda wa miaka 40, watu wanaopenda sanaa waliguswa sana na mahali hapa. Hagia Eirin kwa wakati huu litakuwa jengo lililochaguliwa kuwa nyumba ya kutumbuizia katika tamasha la muziki wa jazz liliandaliwa kukutanisha mataifa tofauti 16. hapa ndo tumefikia mwisho wa maelezo yetu juu ya kanisa la Hagia Eirin kwa siku ya leo.
Jiunge nasi wakati mwingine muda kama huu katika kipindi chetu hiki cha Utamaduni wa Istanbul kwakheriniiii.


Tagi:

Habari Zinazohusiana