UTAMADUNI NA MILA ZA UTURUKI

UTAMADUNI NA MILA ZA UTURUKI WAKATI WA SIKUKUU YA MFUNGO WA RAMADHANI

352284
UTAMADUNI NA MILA ZA UTURUKI

Mwezi wa Ramadhani unamaanisha kuwasaidia wale wasiokuwa na uwezo,kupeana zawadi,kula kwa pamoja katika meza moja, kufunga kiroho na kimwili.mwezi wa Ramadhani unakaribia kikomo jambo ambalo tunalitegemea kukutana nalo ni kusheherekea “sikukuu ya Eid El Fitri”Katika kipindi cha utawala wa Ottoman maandalizi ya sikukuu ya Eid El Fitri katika majumbani,mikoani, na Ikulu yalikuwa yakianza siku chache kabla ya sikukuu kuanza.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya kihistoria: kabla ya siku ya sikukuu maaskari na maafisa hupewa nyongeza katika mishahara yao kama zawadi ya sikukuu. Hata ya kipindi ambacho serikali inakuwa katika wakati mgumu wa kifedha basi mishahara hupunguzwa hadi kufikia nusu ili kuweza kutoa nyongeza au sadaka ya sikukuu hii. Siku ya kwanza ya sikukuu halwa husambazwa katika magereza na kupewa wafungwa. Kutokana na sikukuu wafungwa walionyesha tabia nzuri husamehewa theluthi mbili ya hukumu yake.

Kutoka karne ya 15 kulianzishwa mpangilio na itifaki ya mipango maalumu ya Eid. Kulikuwa na mpango maalumu wa kuadhimisha Eid katika jumba la Ikulu.. Siku ya usiku wa kwanza wa Eid ulinza na kula daku katika jumba la Ikulu na siku ya mwisho ya siku ya ila huswali swala ya alaasiri huswaliwa katika nyumba ya Ikulu.swala la Sultani kwenda na kurudi kutoka msikitini kwa ajili ya swala ya Eid, kilikuwa kikiitwa “maandamano ya Eid” . Sala ya Eid ilikuwa kawaida kufanywa katika moja ya misikiti mikubwa iliyokuwa karibu na Hagia Sophia au msikiti wa Sultanahmet.

Msikiti ambao utasalisha watu katika sikukuu ya Eid, sultani alikuwa akienda kuchagua na kukagua mwenyewe.Baada ya swala ya Eid sultani alipokuwa akirudi nyumbani kwake hapo ndipo maandamano ya Eid huanza,yaani katika maandamano hayo Sultani alikuwa akiwapa mikono na kuwatakia sikukuu njema wafanyakazi wake. Sultani alikuwa akienda katika nyumba ya Hurem kwa ajili ya kubusu mkono wa Sultani Walid. Nyumbani hapo alianza kubusu mkono wa mama yake,na baadae huwatakia sikukuu njema ndugu zake na watoto katika nyumba hiyo. Kisha Sultani huingia katika “ chumba cha chake cha siri” na kukaa katika kiti cha enzi kilichopo mbele ya jumba la Ottomon.

Na kupokea pongezi kutoka kwa wananchi. baada ya pongeze huanza kula chakula na kufurahia sikukuu ya Eid. Masultani wa Ottoman, baadhi ya sikukuu huandaa tamasha kubwa la sherehe kwa wananchi. Tamasha hili ni mchanganyiko wa sultani na watu,hali hii ni muhimu sana ili kuhakikisha ushirikiano wa watu.

Sultani mara nyingine huandaa majengo ya kusheherekea sikukuu kwa watoto.Katika jiji la Istanbul, kuna sehemu tofauti tofauti zilizojengwa kwa ajili ya watoto katika siku za sikukuu, watoto huenda hapo kwa ajili ya kufurahia michezo, na pia kubembea na kucheza michezo mingine mingi katika majengo hayo. Kulikuwa pia na maonyesho ya tamaduni za zamani kama vile karagoz na hajiwat,kula halwa za pamba na pipi za rangi tofauti tofauti.

Maandalizi yaliyokuwa yakiandaliwa kwa ajili ya wananchi huendelea mpaka wa leo.Kwa upande wa majumbani, maandalizi ya sikukuu ya Eid manyumbani yalichukua nafasi kubwa kwa wanawake wa nyumbani.

Maandalizi hayo huanza kwa kufanya usafi.

Baada ya usafi, wakinamama huwaandalia watoto wao nguo maalumu kwa kuwanunulia nguo mpya kwa ajili ya sikukuu. Maandalizi kwa watoto yalikuwa yakitiliwa maanani sana. Enzi za zamani katika jiji la Istanbul, siku ya afara mabafu ya kituruki yalikuwa yakikaa wazi mpaka asubuhi. Siku ya Araf ilikuwa ni mila kwa kila mtu kwenda kujikosha katika mabafu hayo. Mila hii ilkuwa ikiitwa “maji ya Arafa”. Kutokana na maandalizi makali ya sikukuu, baadhi ya wafanyakazi wengine huwa na kazi nyingi kuliko siku nyingine, kama vile wauza pipi na zawadi, washonaji, vinyozi, waokaji, washona viatu ni miongoni mwa makundi ya wafanyakazi hao.

Moja ya jambo la muhimu sana katika siku ya sikukuu ni vyakula.katika kila jiko huandaliwa vyakula na vinywaji maalumu kwa ajili ya sikukuu. Katika jumba la Ikulu vyakula vya sikukuu vilikuwa vikitengwa katika sahani maalumu za kioo. Wageni hupewa ikramu ya maji ya sharubati yenye ubaridi wa barufu zilizowekwa katika glasi za vinywaji hivyo. Kutokana na kufunga kwa mwezi mzima wa Ramadhani vyakula vya sukari hutolewa kwa wageni kama ikramu kubwa katika siku za sikukuu. Vyakula hivyo vya sukari ni kama vile baklava, mkate wa sukari,revani,halva na ashura.

Ziara za makaburini hufanyika siku moja kabla ya sikukuu yaani siku ya Arafa.Waendao katika makaburi huomba dua,kusafisha makaburi, kusoma kur-an, na kumwagilizia maji makaburi.
Moja ya mila ya zamani na mpaka wa leo kufanyika ni wapiga kula daku.

Siku moja kabla ya sikukuu wapiga kula daku huwaamsha watu alfajiri kwa ajili ya sala ya Eid. Wanaume kwenda msikitini, wakiwemo watoto.watu wanaotoka msikitini baada ya swala huanza kupeana mikono ya Eid.Na wakirudi katika majumbani kwao hupeana mikono ya Eid na familia zao. Watoto kuwabusu mikono wakubwa zao na kupewa baashishi na zawadi za Eid. Baada ya kula chakula cha asubuhi watoto huvalia nguo zao mpya na kutembelea majirani.

Matembezi hayo ni kwa ajili ya kupewa zawadi na hela za sikukuu. Ndugu na jamaa hutembeleana, wale wadogo huenda kuwatembelea wakubwa kwa ajili ya kubusu mikono kama mila za kituruki wakati wa sikukuu.Watu wanaokuja kwa ajili ya matembezi ya sikukuu hukaribishwa kwa kupewa ikramu ya sikukuu ya Eid.

Kwa ujumla hupewa ikramu za vyakula vilivyoandaliwa maalumu kwa ajili ya sikukuu.Baada ya chakula huandaliwa kahawa ya kituruki. Siku kuu ya Eid hupewa jina la “Sikukuu ya zawadi za peremende” na hii ndio sababu ikramu za sikukuu hii huwa za vyakula vya sukari.

Kipindi cha sikukuu watu hupatana na kusahau chuki walizokuwa nazo baina yao.

Siku ya sikukuu ni siku za watu waliokosana kusameheana na kwa wale waliopoteana kwa muda mrefu kutembeleana.Mwezi wa Ramadhani ni mwezi uliojaa baraka kwa kila mtu.


Tagi:

Habari Zinazohusiana