Ongezeko la mauzo ya nje ya Uturuki kwa Libya

Uturuki yarekodi ongezeko kubwa la mauzo ya nje kwa nchi ya Libya mwaka huu

1639950
Ongezeko la mauzo ya nje ya Uturuki kwa Libya

Wakati mauzo ya nje ya jumla ya Uturuki yaliongezeka kwa asilimia 33.1 katika kipindi cha Januari-Aprili, ongezeko hili lilifikia asilimia 58 ya mauzo kwa Libya, ambalo ni karibia mara mbili ya wastani wa jumla.

Kiwango cha ongezeko la Aprili kiliongezeka hadi asilimia 228 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Bodi ya Uhusiano wa Kiuchumi ya Kigeni (DEIK) ya Uturuki na Libya Murtaza Karanfil, alisema kuwa serikali ya mpito nchini Libya inaendelea kuona athari nzuri za maslahi ya wawekezaji wa Uturuki katika biashara kati ya nchi hizo mbili.

Akibainisha kuwa walifikia dola milioni 826 na ongezeko la asilimia 58 la mauzo ya nje katika kipindi cha Januari-Aprili, Karanfil alisema kuwa ongezeko kubwa zaidi lilifanywa mwezi uliopita.

Karanfil pia aliripoti kuwa mauzo kwenda Libya mnamo Aprili yaliongezeka kwa asilimia 228 ikilinganishwa na kipindi kama hicho cha mwaka uliopita na kufikia dola milioni 263.3, na kwamba mwelekeo mzuri katika uhusiano wa nchi mbili unaonekana wazi kwenye biashara.

Usafirishaji wa Uturuki kwenda Libya uliongezeka kwa asilimia 58 katika miezi 4 ya kwanza ya mwaka ikilinganishwa na kipindi kama hicho cha 2020, na kufikia dola milioni 826.Habari Zinazohusiana