THY yadumisha uongozi Ulaya

Shirika la ndege la Uturuki (THY) laendelea kuongoza Ulaya kwa wastani wa safari 504 za ndege kwa siku

1636971
THY yadumisha uongozi Ulaya

Shirika la ndege la Uturuki (THY) lilidumisha uongozi wake barani Ulaya kwa wastani wa safari 504 za ndege kwa siku mnamo Mei 6.

Kulingana na ripoti ya trafiki ya ndege ya Shirika la Usalama wa Udhibiti wa Anga barani Ulaya (EUROCONTROL), THY ilipiku wapinzani wake wa Ulaya kwa wastani wa safari 504 za ndege kwa siku.

Air France ilifuata THY katika nafasi ya pili kwa safari 392 za ndege.

Nafasi ya tatu ilishikiliwa na Lufthansa kwa safari 377 za ndege, Wideroe nafasi ya nne kwa safari 344 za ndege, KLM nafasi ya tano kwa safari 304 za ndege na DHL Express nafasi ya sita kwa safari 293 za ndege.Habari Zinazohusiana