Mnada wa sarafu za Bitcoin Ufaransa

Ufaransa kuuza mnadani sarafu za Bitcoin zilizokamatwa na serikali kwa mara ya kwanza

1596698
Mnada wa sarafu za Bitcoin Ufaransa

Nchi ya Ufaransa kwa mara ya kwanza itauza sarafu za Bitcoin kwenye mnada.

Katika mnada utakaofanyika Machi 17, jumla ya sarafu 611 za Bitcoin zilizoibwa na wadukuzi na baadaye kukamatwa na serikali zitauzwa.

Thamani ya sarafu hizo za Bitcoin zitakazonadiwa mnadani ni takriban euro milioni 30.

Wateja ambao watataka kushiriki kwenye mnada huo watalipa ada kuanzia euro 1,500 hadi 10,000 wakati wa usajili na watahitaji kuwa na mikoba ya hifadhi ya kidigitali ili kufanyiwa uhamisho.

Siku moja kabla ya mnada, bei ya chini kabisa itawekwa kwa uuzaji wa sarafu hizo.

Waandaaji wa mnada huo ambao ulipangwa kufanyika mwaka mmoja uliopita lakini ikashindikana  kwa sababu ya taratibu za urasimu, wamefurahishwa na ucheleweshaji huu. Kwa sababu mwaka mmoja uliopita, Bitcoin ilikuwa na karibia moja ya kumi ya thamani yake ya sasa.

Mnada wa Bitcoin ulifanyika Marekani mwaka jana na sarafu 4,000 za Bitcoin zilizokamatwa na FBI (Ofisi ya Serikali ya Upelelezi) ziliuzwa.Habari Zinazohusiana