Uchumi wa Uturuki wakua kwa asilimia 5.9

Uturuki ni moja ya nchi zilizokua kiuchumi licha ya janga la afya kuathiri ulimwengu mzima

1592682
Uchumi wa Uturuki wakua kwa asilimia 5.9

Waziri wa Hazina na Fedha Lütfi Elvan, alisema kuwa Uturuki imekuwa moja ya nchi adimu zilizoweza kufunga mwaka 2020 kwa ukuaji licha ya janga la afya kuathiri ulimwengu mzima.

Taasisi ya Takwimu ya Uturuki (TÜIK), Uturuki ilitangaza takwimu za ukuaji katika robo ya 4 ya mwaka 2020.

Kulingana na takwimu hizo, Pato la Taifa (GDP) liliongezeka kwa asilimia 1.8 mnamo mwaka 2020.

Pato la Taifa liliongezeka kwa asilimia 5.9 katika robo ya 4 ya mwaka 2020 ikilinganishwa na robo hiyo hiyo ya mwaka uliotangulia.

Akitathmini takwimu za ukuaji wa mwaka 2020, Waziri wa Hazina na Fedha, Lütfi Elvan alisema,

"Sisi ni moja ya nchi adimu ambazo zilifunga mwaka 2020 kwa ukuaji licha ya janga la afya ulimwenguni."

Waziri Elvan alitoa taarifa kwenye Twitter na kusema,

"Lengo letu kuu katika mwaka wa 2021 ni kuhakikisha wastani wa bei. Sera zetu za kupambana na mfumko wa bei zitafungua njia bora na uwekezaji endelevu, uzalishaji na njia ya ukuaji zaidi.”Habari Zinazohusiana