Marekani kuuza makombora ya thamani ya dola milioni 990 kwa Australia

Wizara ta mambo ya kigeni ya Marekani imeidhinisha mauzo ya thamani ya dola milioni 990 ya makombora dhidi ya meli kwa Australia

Marekani kuuza makombora ya thamani ya dola milioni 990 kwa Australia

Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani imeidhinisha mauzo ya idadi ya  makombora 200 dhidi ya meli  yenye thamani ya dola milioni 990 kwa taifa la Australia.

Kituo cha mashirikiano ya ulinzi na usalama nchini Marekani kimetoa taarifa kwamba,

 

"Wizara ya mambo ya nje imeidhinisha mauzo kwa Australia ya makombora ya masafa marefu 200 dhidi ya meli aina  AGM-158C pamoja na vifaa vinavyohusiana. Thamani ya mauzo hayo ni dola milioni 990",

Ili mauzo hayo yafanyike inahitajika bunge la Kongresi lisiweke pingamizi lolote ndani ya siku 30.Habari Zinazohusiana