Fed: " Vita vya kibiashara vya Trump vyaiathiri Marekani"

Utafiti uliofanywa na benki kuu ya Marekani (Fed) umebaini kwamba ushuru wa dhiada ulioletwa na Rais Trump kwa bidhaa kutoka mataifa mengine umepelekea kupanda kwa bei na kupotea kwa ajira nchini humo

Fed: " Vita vya kibiashara vya Trump vyaiathiri Marekani"

Katika utafiti uliofanywa na benki kuu ya Marekani (Fed), imebainika kwamba ushuru mpya ulioletwa na Rais Trump kwa kisingizio cha kulinda viwanda vya ndani imepelekea idadi ya ajira kupungua nchini humo pamoja na bei ya bidhaa kupanda.

Matokeo ya utafiti uliofanywa na wachumi wa Fed, Aaron Flaaen na Justin Pierce  uliopewa jina “Madhara ya ushuru wa kidunia 2018-2019 katika sekta ya uzalishaji nchini Marekani” yamechapishwa katika wavuti wa benki hiyo.

Kwa mujibu wa utafiti huo, ushuru wa ziada ulioletwa na Rais Trump mwaka 2018 katika bidhaaza chuma na chuma cha pua kutoka nchi nyingine, umelekea ajira viwandani kupungua hali kadhalika kupanda kwa bei za bidhaa masokoni.

 


Tagi: Trump , Fed , Marekani

Habari Zinazohusiana