Urusi yailipa fidia Ukraine

Shirika la nishati la Urusi la Gazprom limelipa dola bilioni 2.9 kwa shirika la gesi asilia la Ukraine Naftogaz

Urusi yailipa  fidia  Ukraine

Kama adhabu shirika la nishati la Urusi, Gazprom limelipa kiasi cha dola bilioni 2,9 kwa shirika la gesi asilia la Ukraine, Naftogaz.

Taarifa iliyotolewa na Gazprom inasema katika kutekeleza hukumu iliyotolewa na  mahakama ya utatuzi wa migogoro ya kibiashara ya Stockholm shirika hilo limelipa dola bilioni 2.9 kwa shirika la Naftogaz.

Taarifa ya Naftogaz inasema, "Kama ilivyoamuliwa katika mahakama ya biashara ya Stockholm mwaka 2018, tunathibitisha kupokea dola bilioni 2,9 kutoka  Gazprom. Kiasi hicho  kinajumuisha dola bilioni 2,56 kama fidia na kiasi chengine ni riba".

Naftogaz,  waliishitaki Gazprom kwa kushindwa kutekekeleza makubaliano yao ya kibiashara, na kudai lilipwe fidia ya dola bilioni 17.

Kutokana na Gazprom kushindwa kulipa kwa wakati baadhi ya mali zake barani Ulaya zilikamatwa.Habari Zinazohusiana