Helikopta ya kivita iliyoboreshwa yaruka kwa mara ya kwanza kwa mafanikio

Helikopta ya kivita "Atak" iliyotengenezwa na kufanyiwa maboresho Uturuki imefanya safari ya kwanza ya majaribio kwa mafanikio

Helikopta ya kivita iliyoboreshwa yaruka kwa mara ya kwanza kwa mafanikio

Shirika la elimu ya urubani na mambo ya anga (TUSAS) limetekeleza kwa mafanikio jaribio la kwanza la kurusha  helikopta ya kivita iliyotengenezwa na shirika hilo la Uturuki iliyopewa jina Atak.

Waziri wa viwanda vya ulinzi katika ofisi ya Rais, İsmail Demir, ametangaza kupitia ukurasa wa mtandao wa  kijamii,

“ Sehemu ya pili ya maboresho ya kielektronik ya helikopta Atak imekamilika na safari ya kwanza ya majaribio ya helikopta hiyo imefanyika kwa mafanikio, majaribio yote na maboresho yakikamilika helikopta hizo zitatolewa kwa matumizi mwaka 2020 katikati”

Sehemu ya pili ya maboresho ya Atak itakapokamilika helikopta 21 zitakabidhiwa kwa jeshi la Uturuki.


Tagi: Atak , Uturuki

Habari Zinazohusiana