Ujumbe wa Trump kwa shirika la Boeing

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa ushauri kwa shirika la kutengeneza ndege la Boeing kuhusiana na ndege zake za B 737 Max

Ujumbe wa Trump kwa shirika la Boeing

Rais wa Marekani Donald Trump alishauri shirika la Boeing kufanya mabadiliko katika ndege zake aina ya 737 Max na kuja na jina jipya kwa ndege hizo. Hiyo inafuatia nchi nyingi dunia kupiga marufuku matumizi ya ndege hizo baada ya kutokea ajali inayoihusisha ndege hizo Indonesia na Ethiopia.

Trump alitoa ushauri huo kupitia ukurasa wake binafsi wa Twitter ambako pia aliandika maneno ya kushangaza akisema yeye hajui chochote kuhusiana na masuala ya chapa za kibiashara lakini kama Rais anatoa ushauri wake.Habari Zinazohusiana