Siasa na Uchumi

Uwekezaji katika teknolojia ya kiwango cha juu ni muhimu kama ilvyo muhimu kutafuta masoko mapya katika kukuza biashara ya nje

Siasa na Uchumi

Biashara ya nje ni moja ya maeneo yalioathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na kuyumba kwa bei za kubadilisha fedha za kigeni kulikotokea mwezi August.Ukiangalia uhusiano uliopo baina mabadiliko ya bei ya kubadilisha fedha za kigeni na taarifa ya biashara ya nje, ni vema kuweka wazi kwamba uhusiano huo ni hasi unapoangalia manunuzi ya nje, ilhali ni chanya unapoangalia mauzo.

Ni kusema kwamba bei ya kubadilishia fedha inapoongezeka, mapato yanayotokana na mauzo hayo ya nje nayo pia huongezeka. Ongezeko hili sio swa kwa yule anayetumia malighafi kutoka nje, kwa sababu bei ya kubadilisha fedha inapoongezeka gharama ya uzalishaji nayo pia huongezeka. Hii pia ni sababu ya gharama za manunuzi kutoka nje kuongezeka, pia ni sababu ya manunuzi kuchelewa

Je kuyumba huko kwa bei kulikodumu kwa miezi kadhaa ambako Uturuki imepitia kunajiakisi vipi katika uchumi ?

Mkufunzi katika idara ya Uchumi kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Yildirim Beyazit, Prof. Dr. Erdal Tanas KARAGÖL  anaelezea...

 Mnamo mwezi Oktoba uchumi wa Uturuki kwa upande wa biashara ya nje ulipitia kipindi muhimu sana mara  baada ya kuongezeka kwa bei ya kubadilisha fedha. Kwa taarifa  ni kwamba mauzo ya nje ya Uturuki kipindi cha mwezi Oktoba yamevunja rekodi ya nchi. Mwezi Oktoba mauzo ya nje yalikuwa ni dola bilioni 15.7. Jumuisho la mauzo kwa miezi 12 mpaka kufikia kipindi hiko linakuwa dola bilion 166.8. Mnamo mwezi Oktoba Ukilinganisha kiwango cha  mauzo na manunuzi ni asilimia 96.7, hii inaonyesha utendaji wa ufanisi mkubwa.

 Katika msawazo wa biashara ya nje kuboreka huku, ukilinganisha na uchelewaji wa manunuzi, Ongezeko hili la mauzo linaakisi maendeleo chanya yaliyotokea katika uchumi.

  Inapozungumziwa  mauzo pamoja na uimarishwaji wa mauzo hayo ni dhahiri mchakato huu utachangia kwa kiasi kikubwa katika kuweka msawazo wa kiuchumi iwe kwa ongezeko la la bei ya fedha za kigeni au kwa kuimarika kwa bei hizo. Pia ili kuweza kudumisha mauzo ya nje inabidi kupunguza utegemezi wa malighafi kutoka nje. Hili litaongeza ufanisi katika uzalishaji kwa upande mmoja na kwa upande mwingine litapunguza nakisi ya biahsara ya nje na mwishowe kupunguza nakisi ya fedha za kigeni.

 Kasi hii tuliyofikia sasa katika mauzo ya nje ili iweze kudumu  inatupasa kuwa na muundo utaowezesha hili, na wakati wa kutengeneza muundo huo ni sasa. Mauzo inabidi yahimizwe ndani ya nchi na kimataifa kwa wafanyabiashara wa aina zote, hivyo ni wajibu kwa mamlaka husika kutoa fursa za kutosha pamoja unafuu kwa kila mfanyabiashara bila kuangalia ana uwezo kiasi gani.

Ili kuweza kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kimataifa inabidi kuendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji. Kuwawezesha wawekezaji wa nje kuwekeza ni jambo la kutilia mkazo.

Cha msingi zaidi ni kupunguza gharama za uzalishaji, kuwezesha mazingira ya ushindani kibiashara na kubwa zaidi ni kushusha viwango vya gharama za riba.

 Je ni bidhaa gani inatupasa ziuzwe nje ? na inawezekanaje kufikia kiwango cha juu kabisa cha uuzaji wa nje wa bidhaa ?  Kama inavyofahamika majibu ya maswali haya ni ziada ya kinachozalishwa. Na ili ipatikane ziada katika uzalishaji yapasa makampuni yote yazalishe ziada, yapasa maeneo mapya ya uwekezaji yavumbuliwe.

 Katika malengo ya muda wa kati yote hayo ni muhimu sana. Ila inabidi kufahmu yafuatayo.Katika uchumi wa kidunia kuna garimoshi ya kiteknolojia linlokwenda kwa kasi ya ajabu.kila hatua tunayopiga katika utafiti na uendelezaji, Ubunifu, teknolojia ya kisasa inatusaidia kuendana na mwendo kasi wa  garimoshi hilo.

Unapoangalia uwekezaji wa kisasa kitu muhimu kabisa ni kuchochea uwekezaji uliojikita katika teknolojia. Inapasa kuchochea uwekezaji katika teknolojia. Kiasi cha uwekezaji kwenye teknolojia ukilinganisha na uwekezaji wote uliopo inabidi kiongezeke.

Hivyo basi ili kuandika historia mpya katika mauzo ya nje ya Uturuki kitu muhimu kabisa kama ilivyo katika kuvumbua masoko mapya ni uwekezaji katika teknolojia ya kisasa ya viwango vya juu.

Mkufunzi katika idara ya Uchumi kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Yildirim Beyazit, Prof. Dr. Erdal Tanas KARAGÖL.

 Habari Zinazohusiana