Mataifa 16 yaungana dhidi ya Marekani

Wakati Marekani ikiwa katika mpango wa kuongeza ushuru kwa bidhaa za China,mataifa kumi na sita yanaungana kibiashara dhidi yake

Mataifa 16 yaungana dhidi ya Marekani

Wakati Marekani ikiwa katika mpango wa kuongeza ushuru kwa bidhaa za China,mataifa kumi na sita yanaungana kibiashara dhidi ya Marekani.

Mpango wa kufanya biashara bila Marekani upo mbioni kukamilika.

Mataifa kumi na sita ya Asia Pasifiki yameungana na kutengeneza mpango utakaochukua nafasi kubwa katika biashara ya kimataifa.

Nchi zilizo katika mpango huo ni China, Japan, Korea Kusini, India, Australia, New Zealand, Indonesia, Ufilipino, Cambodia, Laos, Malaysia, Brunei, Myanmar, Singapore, Thailand na Vietnam.

Nchi husika zitahakikisha zinasuluhisha matatizo na migogoro yoyote iliyo kati yao ili kuwezesha mafanikio ya kibiashara.

Mkataba huo utaegemea zaidi katika kufanya biashara na China na TPP(Trans Pacific Partnership) bila ya Marekani.

Hali kadhalika Trump kwa upande wake ametangaza kuwa haoni haja ya Canada kuendelea kuwepo katika Mkataba wa Biashara ya Huru ya Amerika ya Kaskazi NAFTA(North American Free Trade).

Trump katika ukurasa wake wa twitter ameandika kuwa,"Baada ya miaka mingi ya unyonyaji,iwapo hatutafikia makubaliano yatakayoinufaisha Marekani basi Canada inatolewa katika NAFTA".

Donald Trump amendika ujumbe mwingine akilionya bunge la Marekani kutoingilia mazungumzo hayo la sivyo ataufutilia mbali kabisa mkataba wa NAFTA.Habari Zinazohusiana