Uturuki kuongeza uzalishaji wa nishati mbadala

Uturuki imepitia mpango wake wa nishati mbadala wa mwaka 2023 kwa lengo la kuongeza uwezo wa uzalishaji wa nishati safi kutoka asilimia 31 mpaka asilimia 50

Uturuki kuongeza uzalishaji wa nishati mbadala

Uturuki imepitia mpango wake wa nishati mbadala wa mwaka 2023 kwa lengo la kuongeza uwezo wa uzalishaji wa nishati safi kutoka asilimia 31 mpaka asilimia 50 kufikia mwaka 2023.

Mwezi wa tano mwaka 2018, msimamizi mkuu wa sekta ya nishati nchini Uturuki alisema kuwa uwezo wa uzalishaji umeme uliokuwepo umeongezeka kwa asilimia 181 kutoka megawati 32 mpaka kufikia megawati 90 kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita.  

Kufikia mwezi wa tano uwezo wa umeme mbadala ulifikia asilimia 46 kati ya jumla ya nishati mbadala iliyopo wakati uzalishaji wa umeme mbadala ulifikia asilimia 30.

Kutokana na mpango kazi wa nishati mbadala wa Uturki wa mwaka 2013, uwezo wa umeme mbadala ulikua asilimia 29 na uwezo wa jumla ya nishati mbadala iliyopo ulikua asilimia 40

Baada ya kufikia lengo la asilimia 31 ya uzalishaji wa umeme mbadala mwaka 2018, Mamlaka za nishati za Uturuki zilichukua hatua stahiki za kupitia mpango wake wa nishati mbadala wa mwaka 2023.

Tarehe 3 mwezi wa nane , Raisi wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alizindua siku 100 za kuandaa mpango kazi wa kuendeleza sekat nishati nchini kwa kutumia maliasili za nchi kama upepo, jua na mvuke wa maji.

Kama sehemu ya siku 100 za mpango kazi , Uturuki imepanga kuwekeza takribani dola bilioni 4.8  kwenye nishati mbadala, imekusudia  kutoa zabuni mbalimbali ikiwemo zabuni ya kusimika mitambo ya kuzalisha umeme wa jua yenye uwezo wa gigawati 3

Uturuki imepanga pia kukuza uwezo wake kuzalisha nishati ya upepo na jua kufikia megawati 10,000 kila moja

Wizara ya nishati na maliasili ya Uturuki itaanza kupokea maombi ya zabuni ya kusimika mitambo mikubwa ya kuzalisha nishati kwa njia ya upepo yenye uwezo wa megawati 1200 ambayo itakua mitambo mikubwa kuhawi kutokea.

Miongoni mwa masharti ya zabuni hiyo yanaitaka kampuni itakayoshinda zabuni asilimia 60 ya vifaa vitavyotumika viwe vinatoka ndani ya nchi na asilimia 80 ya wakandarasi watakao ajiriwa wawe na asili ya Uturuki

Saros na Gallipoli ndio maeneo yaliyochaguliwa kusimika mitambo hiyo maeneo hayo yanayopatikana mkoa wa Marmara na Kiyiköy.

 Habari Zinazohusiana