Qatar kuwekeza kiwango cha dola bilioni 15 nchini Uturuki

Amir wa Qatar Sheikh Tamim ben Hamad Al Thani afahamisha kuwa Qatar itawekeza kiwango cha dola bilioni 15 nchini Uturuki

Qatar kuwekeza kiwango cha dola bilioni 15 nchini Uturuki

Amir wa Qatar Sheikh Tamim ben Hamad Al Thani afahamisha kuwa Qatar itawekeza  kiwango cha dola bilioni 15 nchini Uturuki  katika ziara yake aliofanya nchini Uturuki na kuzungumza na rais Erdoğan.

Amir wa Qatar alipoklewa  na rais wa Uturuki  katika ziara yake mjini Ankara.

Taarifa kutoka ikulu mjini Ankara zimefahamisha kuwa  mazungumzo kati ya rais wa Uturuki na amir wa Qatar Tamim ben Hamad Al Thani  yalichukuwa muda wa  masaa matatu na nusu bila ya waandishi wa habari kuhudhuria.

Katika mazungumzo yo kulizungumziwa pia  ushirikiano uliopo baina ya mataifa hayo mawili na  masuala tofauti ya kikanda.

Rais wa Uturuki na amir wa Qatar wamefahamisha kuwa malengo yao ni mataifa hayo mawili  kuzidi kushirikiana katika sekta tofauti.

 Habari Zinazohusiana