Teksi ya kwanza ya umeme ya angani

Marekani yatambulisha teksi ya kwanza ya umeme inayoruka angani

1656331
Teksi ya kwanza ya umeme ya angani

Teksi ya kwanza ya umeme inayoruka angani  "Maker" iliyotengezwa Marekani (USA), imetambulishwa.

Picha za teksi hiyo inayoruka angani pia zilichapishwa wakati wa kutambulishwa rasmi.

Teksi hiyo inayobeba watu wawili itaweza kuruka kwa mwendo wa kasi ya kilomita 240 kwa saa.

Lengo la utengenezaji wa teksi hiyo inayoruka ni kupunguza safari ya saa moja katika msongamano wa trafiki hadi dakika 5.

Safari ya kilomita 30 kwa kutumia teksi hiyo itagharimu dola 70.

Teksi hiyo ambayo bado liko katika hatua ya majaribio, inatarajiwa kupokea vyeti kutoka kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Marekani ifikapo mwaka 2024.Habari Zinazohusiana