Mpango wa Instagram ya watoto wakosolewa

Mark Zuckerberg akosolewa na mashirika ya umma kwa mpango wa uanzilishi wa Instagram ya watoto

1622766
Mpango wa Instagram ya watoto wakosolewa

Programu ya mtandao wa kijamii ya Instagram inayomilikiwa na Facebook, inafanya maandalizi ya toleo jipya la Instagram kwa ajili ya kuruhusu watoto walio chini ya umri wa miaka 13 kutumia.

Msemaji wa Facebook Stephanie Otway alisema kuwa kampuni hiyo haitaonyesha matangazo kwenye programu zinazolenga watoto walio chini ya umri wa miaka 13, na Facebook itashauriana na wataalam juu ya afya na usalama wa watoto ili kuifanya programu hiyo iweze kutumika kwa usalama zaidi.

Wakati huo huo, uanzishwaji wa jukwaa linalofanana na Instagram ambapo watoto walio chini ya umri wa miaka 13 wanaweza kuchapisha picha zao ulikosolewa na mashirika ya umma.

Mashirika kadhaa ya utetezi wa haki za watoto yalituma barua kwa Mark Zuckerberg, mwanzilishi wa Facebook, wakimhimiza kufuta mipango yao, huku wakionya kuwa hii itawaweka watoto katika hatari kubwa.Habari Zinazohusiana