Kituo cha kwanza cha Twitter Afrika

Twitter kufungua kituo cha kwanza barani Afrika katika nchi ya Ghana

1620340
Kituo cha kwanza cha Twitter Afrika

Mtandao wa kijamii wa Twitter utafungua ofisi yake ya kwanza barani Afrika katika nchi ya Ghana.

Mkurugenzi Mkuu wa Twitter Jack Dorsey, alitoa taarifa kwenye akaunti yake ya Twitter na kusema,

"Twitter sasa inapatikana katika bara la Afrika. Tunatoa shukrani kwa Ghana na Nana Akufo-Addo."

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo alisema kuwa hii ni habari njema kwamba Twitter ilichagua Ghana kama kitovu cha shughuli zake za Afrika.

Akufo-Addo aliongezea kusema kuwa serikali na wananchi waliridhika kupokea taarifa hizo na kwa uaminifu wa Ghana.Habari Zinazohusiana