Zuckerberg adaiwa kutumia programu ya Signal

Mmiliki wa WhatsApp na Facebook Mark Zuckerberg adaiwa kutumia programu pinzani ya Signal

1616770
Zuckerberg adaiwa kutumia programu ya Signal

Mark Zuckerberg ambaye ni mmiliki wa WhatsApp na Facebook, anadaiwa kutumia Signal ambayo ni programu pinzani ya mawasiliano.  

Mtafiti wa usalama anayeitwa Dave Walker, alidai kwamba mkurugenzi mkuu wa Facebook Mark Zuckerberg alikuwa akitumia programu ya Signal kwa sababu ya hofu ya usalama wa data.

Akikumbusha kwamba data za mamilioni ya watumiaji wa Facebook zilidukuliwa na kuvujishwa kwenye, Walker alidai kuwa data za Zuckerberg pia zilikuwa miongoni mwao.

Walker alidai kwamba Zuckerberg alipendelea kutumia Signal ambayo ni programu hasimu ya mawasiliano ya ujumbe ili kulinda faragha dhidi ya ukiukaji wa data.

Hakukuwa na taarifa yoyote ya ukanushaji juu ya suala hili kutoka upande wa Zuckerberg.

Facebook, ambayo ilianzishwa na Mark Zuckerberg ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji, ilijumuisha programu ya mawasiliano ya ujumbe wa papo hapo ya WhatsApp mnamo mwaka 2014.Habari Zinazohusiana