Nishani ya heshima kwa Özlem Türeci na Uğur Şahin

Waanzilishi wa BioNTech na wazalishaji wa chanjo ya Covid-19 kupewa nishani ya heshima Ujerumani

1591813
Nishani ya heshima kwa Özlem Türeci na Uğur Şahin

Wanzilishi wa kampuni ya BioNTech ya Ujerumani ambayo ilizalisha chanjo ya corona (Covid-19), Dr. Uğur Şahin na Dr. Özlem Türeci, watapewa medali ya heshima nchini Ujerumani.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais nchini Ujerumani, iliarifiwa kuwa katika hafla itakayoandaliwa na Rais Frank-Walter Steinmeier katika Jumba la Bellevue Machi 19 na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Angela Merkel, wanasayansi wa Kituruki Özlem Türeci na Uğur Şahin watakabidhiwa nishani ya heshima ya kufuatia agizo lililotolewa.

Katika taarifa hiyo iliyobainisha kwamba wanandoa hao watafiti na waanzilishi wa BioNTech watapokea nishani ya heshima na kukutana na Rais Steinmeier ambaye ataonana nao uso kwa uso kwa mara ya kwanza mwaka huu, tafiti za matibabu za Özlem Türeci na Uğur Şahin zilielezwa.

Taarifa hiyo pia ilisisitiza kuwa Türeci na Şahin walichangia kuzuia kuzuka kwa Covid-19 na kusema,

"Tunawashukuru kwa uwezo wao uliotambuliwa ulimwenguni katika uwanja wa teknolojia za m-RNA na juhudi zao zisizokuwa na kikomo. Waliweza kuboresha na kuidhinisha chanjo dhidi ya Covid-19 kwa muda mfupi sana."Habari Zinazohusiana