Picha za sayari ya Mars zachapishwa

NASA yachapisha picha za sayari ya Mars zilizonaswa na chombo cha "Perseverance"

1590779
Picha za sayari ya Mars zachapishwa

NASA imechapisha picha ya panoramic iliyotumwa na chombo cha "Perseverance" kwa ajili ya uchunguzi kwenye sayari ya Mars.

Picha hiyo ambayo ilirekodiwa na kifaa cha upigaji picha cha Mastcam-Z kilichojumuishwa katika chombo cha "Perseverance"na kuunganishwa kwa mikusanyiko 142 tofauti, ilichapishwa kwenye wavuti ya NASA.

Chombo cha "Perseverance" kilichozinduliwa kutoka Florida mnamo Juni 30, 2020, kiliweza kutua juu ya sayari ya Mars mnamo Februari 20, baada ya safari ya takriban miezi 7 ya masafa ya kilomita milioni 470.

Chombo cha "Perseverance" kilichoundwa katika Maabara ya Jet Propulsion ya NASA huko California na kinachotumia mafuta ya plutonium, kinatambulika kuwa na vifaa vya hali ya juu zaidi vya kiteknolojia kushinda vyombo vingine vyote vilivyowahi kutumwa Mars hadi sasa.Habari Zinazohusiana