Facebook kuzuia uchapishaji wa taarifa potofu za Covid-19

Facebook na Instagram zitazuia uchapishaji wa taarifa za kupotosha kuhusu Covid-19

1539802
Facebook kuzuia uchapishaji wa taarifa potofu za Covid-19

Shirika la mtandao mkubwa wa kijamii wa Facebook kutoka Marekani, limetangaza kuwa litaondoa taarifa potofu zinazochapishwa kuhusu chanjo za corona (Covid-19).

Katika taarifa iliyotolewa na shirika hilo, iliarifiwa kuwa mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram haitaruhusu uchapishaji wa taarifa zenye madai yaliyokataliwa na wataalam wa afya wa umma.

Katika taarifa hiyo pia iliandikwa,

"Tutaondoa madai ya uwongo juu ya chanjo ya Covid-19 ambayo yanachapishwa kama vile maelezo ya vidonge vidogo, na nadharia zisizokuwa na ukweli kuhusu utumiaji na ufanyaji majaribio bila idhini wala kuzingatia usalama wa chanjo."

Katika taarifa hiyo ambayo imedhihirisha kwamba Facebook iliondoa taarifa karibia milioni 12 zilizokuwa na habari za uwongo kuanzia Machi hadi Oktoba tangu janga la Covid-19 lilipoanza USA, pia zilibainisha kuwepo kwa nakala zilizohimiza ukanushaji wa taarifa potofu kuhusu Covid-19.Habari Zinazohusiana