Youtube kuzuia taarifa za chanjo ya Covid-19

Video zinazochapishwa Youtube zenye maelezo kuhusu chanjo ya Covid-19 kuondolewa

1510438
Youtube kuzuia taarifa za chanjo ya Covid-19

Mtandao wa uchapishaji video wa Youtube, umetangaza kuchukuwa hatua dhidi ya taarifa za kupotosha zinazohusiana na chanjo ya Covid-19.

Kulingana na taarifa za BBC, iliarifiwa kuwa mtandao huo utaruhusu uchapishaji wa taarifa za chanjo ya Covid-19 ambazo zitatoka kwa mamlaka husika za kiafya na shirika la afya duniani WHO.

Maelezo zaidi yanasema, ‘‘Tunahitaji kuwa na sheria sahihi za kuondoa habari za kupotosha mtandaoni hasa katika kipindi hiki ambacho kuna shughuli muhimu za dharura zinazoendelea kwa ajili ya chanjo ya Covid-19.’’

Hapo awali, mtandao wa Youtube ambao upo chini ya shirika la Google, uliwahi kutangaza kuchukua hatua na tahadhari dhidi ya uchapishaji wa ‘maelezo yaliyokosa vyanzo vya kimatibabu’ kuhusu Covid-19.

Hatua hii ya Youtube ilichukuliwa baada ya mtandao wa kijamii wa Facebook kutangaza kuzuia uchapishaji wa matangazo yote yanayohimiza watu kufanyiwa chanjo.

Hata hivyo, hatua iliyochukuliwa na Facebook haijajumuisha uchapishaji wa maelezo yasiyohusisha matangazo, tofauti na Youtube ambayo imejumuisha uchapishaji wa maelezo ya aina yote kuchukuliwa hatua.Habari Zinazohusiana