Chuo kikuu cha Izmir Uturuki chapiga hatua katika kufaanikisha utenegezaji wa chanjo ya Covid-19

Wanasayansi katika chuo kikuu cha Izmir wapiga hatoa yenye matumaini katika utafiki kuhusu chanjo dhidi ya virusi vya corona

1398253
Chuo kikuu cha Izmir Uturuki chapiga hatua katika kufaanikisha utenegezaji wa chanjo ya Covid-19


Wanasayansi katika chuo kikuu cha Izmir wapiga hatoa yenye matumaini katika utafiki kuhusu chanjo dhidi ya virusi vya corona.

Majaribio ya kwanza  ya vimelea  yamefanyika katika maabara ya chuo kikuu cha mkoani Izmir , majaribio ambayo ni moja ya hatua ambazo malaengo yake ni kutengeneza chanjo ya virusi vya corona.

Vimelea vya kinasaba vimefanyika utafiti ili  kufaanikisha mradi huo ambao unalengo kupatikana  kwa chanjo dhidi ya virusi vya corona.

Jopo la watafiti  kuhusu kinga ya virusi katika chuo kikuu cha Egena mkoani Izmir Magharibi mwa Uturuki limefaulu kupiga hatua kwa ushirikiano na taasisi ya TUBITAK, Taasisi inayohusika na utafiti ya kisayansi na teknolojia Uturuki.

Jopo  hilo  limeanza majaribio katika maabara  ya chanjo hiyo.

Wanasayansi 32 kutoka katika maabara tofauti  wanashiriki katika utafiti huo.

Profesa Mert Doskaya amesema kuwa, kuna uwezekano wa kufanya majaribio ya kwanza  ya chanjo ya DNA kwa wanyama  miezi minne ijayo na baadae kutolewa kwa binadamu.
 Habari Zinazohusiana