Watafiti: Virusi vipya vya Corona havijatengenezwa na binadamu

Utafiti uliofanywa na timu ya wanasayansi wa kimataifa umebaini kwamba virusi vipya vya Corona (Covid-19) haviwezi kuwa vimetengenezwa na binadamu

1381529
Watafiti: Virusi vipya vya Corona havijatengenezwa na binadamu

Utafiti uliofanywa na timu ya wanasayansi wa kimataifa umebaini kwamba virusi vipya vya Corona (Covid-19) haviwezi kuwa vimetengenezwa na binadamu. Virusi hivyo vina vyanzo vyake vya kiasili na kupitia njia ya mabadiliko ya kidogo kidogo virusi hivyo vikafanyika.

Katika utafiti uliochapishwa kwenye jarida la “Nature Medicine”, utaifiti huo uliohusu virusi Covid-19 na mfuatano wa dna shirikishi, mfanano katika virusi vingine. Matokeo ya utafiti yalionyesha kwamba hakuna dalili yeyote inayothibitisha kwamba virusi hivyo vilitengenezwa maabara.

Kuhusiana na jinsi gani virusi viliweza kwa mara ya kwanza kumuathiri binadamu. Wanasayansi hao wamesema kwamba huwenda virusi hivi ambavyo vilikuwa vikiathiri popo vilipitia mabadiliko Fulani ya kiasili na kuviwezesha kupata uwezo wa kuathiri binadamu, au inawezekana pia virusi ambavyo vilikuwa havina madhara kwa binadamu vimebadilika vikapara uwezo wa kumuathiri binadamu.

Utafiti huo ulichangiwa na watafiti kutoka vyuo vikuu vya Columbia, Edinburgh na Sydeney.

 Habari Zinazohusiana